BRICS

Na

Omar Abdel-Razek

Moja ya maendeleo hayo ni kuongozeka kwa nchi zinazotengeneza Jumuiya hiyo za nchi zinazoendelea haraka kiuchumi, yaani BRICS, kwa kuwakaribisha Misri, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia, na umoja wa nchi za falme za Kiarabu.

Kwa sasa, ‘BRICS’ inaundwa na Urusi, Brazil, Jamhuri ya Watu wa China, India, na Afrika ya Kusini.

Hii inakuja baada ya jitihada za Argentina kujiunga na umoja huo kushindikana, baada ya nchi hiyo kutoka Amerika ya Kusini kubadili maamuzi yake dakika za lala salama. Kwa wakati huu, BRICS inatajwa kama jumuiya kubwa kuliko zote nay a kwanza kabisa toka Afrika ya Kusini kujiunga nayo mwaka 2010.

Inakadiriwa kuwa, Jumuiya ya nchi za BRICS inawakilisha asilimia 43 ya idadi ya watu duniani na asilimia nyingine 16 ya biashara duniani.

Hapo nyuma, jumuiya hiyo ilitambulika kama BRIC, ufupisho uliobuniwa na Jim O’Neil, mtaalamu wa uchumi kutoka taasisi ya Goldman Sachs mwaka 2001.

BRICS

Hata hivyo, kukua kwa Jumuiya ya BRICS bado kunaibua hisia tofauti, zikiwemo za hofu na matumaini.

Matarajio ya matumaini yanatokana na ukweli kwamba, BRICS itachochea na kuchagiza mabadiliko ya dhana katika uchumi wa nchi zinazoibukia kiuchumi, ambazo hapo awali, zilipigwa dafrau kutoka kwenye soko la mataifa yaliyopiga hatua kiviwanda na vilevile, kulemewa na madeni ya nje.

Uimarisha wa ushawishi wa Afrika

Hatua ya Jumuiya hiyo ya kutokukubali kuafikiana na vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Urusi iliyo vitani dhidi ya Ukraine, na badala yake, kuendelea kufanya mazungumzo na kushiriki kibiashara na nchi hiyo kutoka Ulaya Mashariki na Asia, inatabanaisha mkakati kabambe na wenye dalili za matumaini kati ya umoja wa kisiasa na maslahi ya kiuchumi.

Vilevile, ujio wa Misri na Ethiopia ndani ya BRICS, unazidi kuimarisha ushawishi wa Bara la Afrika ndani ya Jumuiya hiyo.

Hatua hii, pia inaelezwa kufifisha uwakilishi wa Afrika ya Kusini, nchi yenye chumi mdogo kwenye Jumuiya hiyo.

Urusi BRICS

Misimamo ya nchi kutoka bara la Amerika ya Kusini, ingejipambanua wazi ndani ya BRICS, laiti Argentina isingekubali kubadili maamuzi yake ya dakika za mwisho

Wakati dunia inashuhudia mtangamo wa kimataifa, mchanganyiko wa siasa na uchumi, unadhihirisha wazi umuhimu wa umoja wa nchi zinazoendela haraka kiuchumi, kuelekea ushirikishwaji wa makundi na pande nyingi katika siasa za kimataifa, kama inavyochagizwa na nchi waanzilisha wa Jumuiya hiyo, yaani Urusi na Jamuhuri ya watu wa China.

Dhana muhimu inayoshuhudiwa katika mabadiliko haya ni ni uundwaji wa mfumo wenye pande mbili katika maendeleo ya kimataifa, kama inavyodhihirishwa na hatua ya Benki ya NDB, iliyo chini ya BRICS, ya kuidhinisha kiasi cha dola kimarekani 33 bilioni, kwa ajili ya miradi yenye tija kubwa ndani ya Jumuiya ya nchi zinazondelea haraka kiuchumi.

Mfumo mbadala wa Malipo

Kwa sasa, benki ya NDB inaonekana kama muarobaini wa ‘sera za uliberali mamboleo’, dhidi ya ‘nchi za kitropiki’ kutoka mashirika ya Kimataifa kama IMF na yatokanayo kwenye makubaliano ya Washington ya mwaka 1989.

Uamuzi wa Urusi na Jamhuri ya watu wa China wa kuja na pendekezo la kuwepo na mbadala katika mfumo wa ulipaji, kwa hakia umefifisha utawala wa dola ya Kimarakeni na kimsingi, kuruhusu na kuzipa uwezo nchi za BRICS kufanya biashara kwa kutumia sarafu zao wenyewe, na hatimaye kutoa ahueni kwa nchi za Afrika ambazo bado zinaelemewa na mzigo wa madeni ya nje.

Kwa kuridhia ukaribisho wake ndani ya BRICS, nchi ya Misri inategemea kuona upungufu mkubwa wa shinikizo wa fedha za kigeni, hususani, kupitia mpango na lengo la Jumuiya ya nchi zinazoendelea kiuchumi wa kuondoa miamala ya fedha inayotumia dola za Kimarekani.

Ethiopia kwa upande wake, ambayo inatajwa kama nchi inayokuwa kwa kasi kiuchumi barani Afrika, nayo inaangazia fursa kama hiyo, ambayo itaiwezesha nchi hiyo iliyo katika pembe ya Afrika kupiga vita na kupinga mashiniko ya mara kwa mara kutoka nchi za Magharibi, ambayo yameegemea zaidi katika dhana ya ‘haki za kibinadamu’.

Hatua hii inalenga kuinua hadhi ya Ethiopia kimataifa, kulingana na Padraig Carmody, Profesa wa Jiografia kutoka chuo cha Trinity kilichopo Dublin, Ireland, na hivyo kuchagiza ushirikiano wa karibu kati ya Ethiopia nan chi kubwa duniani, lengo likiwa kuvutia uwekezaji zaidi.

Hata hivyo, pamoja na matumaini yote haya, bado changamoto si haba.

Kwa mfano, harakati za muda mrefu zilizolenga kuimarisha ushirikiano wa nji ‘zilizo kusini’, zimeshidwa kufua dafu mbele ya utawala wa muda mrefu wa nchi za Magharibi.

Mpango wa kwanza kabisa ni kizamani haswa, sawa na mkakati kuzikomboa nchi hizo kwenye makucha ya wakoloni.

Hata baada ya mkutano wa kwanza wa nchi za Asia na Afrika uliofanyika mwaka 1955 mjini Bandung nchini Indonesia, bado utaratibu na utawala wa kidunia haujabadilika ambapo utawala wa taasisi na mashirika mbalimbali ya kimataifa ya kifedha bado yanatamalaki.

Ugumu na utofauti

Japokuwa BRICS haiwezi kuwa tishio kundi la G7, linaloundwa na mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa nchi 7 zilizoendelea sana na zinazoongoza kiuchumi duniani, maarufu kama G20, kutokana na lengo lake mahsusi, kuongezeka maradufu kwa idadi yake, bado kunaweza kutishia utawala wa nchi ya Marekani, kulingana na mchambuzi wa masuala ya uchumi kutoka Afrika ya Kusini, Marisa Lourenco.

Uwepo wa changamoto ndani ya BRICS zitokanazo na ukubwa wa Jumuiya yenyewe na uwezo wa kiuhcumi wa Jamuhuri ya watu wa China na India, ukilinganisha na hali dhoofu za Ethiopia na Misiri ambazo bado zinaelea kwenye dimbwi la madeni unaweza ukawa kikwazo cha kuimarika Jumuiya hii na hatimaye kutimiza malengo yake tarajiwa.

Masuala ya Kisiasa kama vile migogoro ya kimipaka kati ya Jamuhuri ya watu wa China na mvutano juu ya umiliki wa matumizi wa bwawa la mto Nile, kati ya Misri na Ethiopia na bila kusahau uhasama katika ghuba ya Uajemi kati ya Saudi Arabia na Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran, ni uthibitisho tosha wa ugumu unaozikabili nchi za BRICS, hata katika hali yake mpya.

Kinadharia, muundo wa nchi za BRICS unatosha kabisa kushughulikia tofauti hizi bila kuathiri miradi ya maendeleo.

Jumuiya ya nchi zinazoendelea haraka kiuchumi, hutegemea Zaidi mikutano yake ya mwaka kama viako muhimio vyenye kutoa maamuzi pasipo uwepo wa aina yoyote ya urasimu.

Mafanikio ya BRICS bado yapo katika majaribio, huku kukiwa na ongezeko la ushindani wa kimataifa kati ya Marekani na washirika wake kwa upande mmoja; Urusi na Jamuhuri ya watu China katika upande mwingine.

Mwandishi wa Makala hii ni mtaalamu wa saikolojia na alipata kufanya kazi kama mhariri katika idhaa ya Kiarabu ya BBC. Kwa sasa anaishi na kufanya kazi London, Uingereza.

Kanusho: Maoni yaliyoonyeshwa na mwandishi hayaakisi lazima maoni, mitazamo, na sera za uhariri za TRT Afrika.

TRT Afrika