Kura iliyopigwa siku ya Ijumaa, ya kuitambua kama mwanachama wa Palestina ilikuwa ni ishara kubwa. Tuwe wakweli tu, pamoja na manufaa yatakayopatikana kutokana na hatua hiyo, je ishara hii italeta mabadiliko yoyote?
Kura hiyo iliyopigwa na nchi 143 ilithibitisha ombi la Wapalestina la kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa.
Licha ya pingamizi kali kutoka kwa Marekani na Israel mwaka 2012, Palestina ilibadilisha hali yake kutoka "chombo kisicho mwanachama wa waangalizi" hadi "nchi ya waangalizi isiyokuwa mwanachama."
Hatua hii iliipa Palestina nafasi ya kujiunga na mashirika ya kimataifa kama vile Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na kufungua kesi dhidi ya makazi ya Wayahudi kinyume cha sheria katika Ukingo wa Magharibi na mashambulizi ya kijeshi katika Ukingo wa Magharibi na Gaza.
Hata hivyo, uanachama kamili katika Umoja wa Mataifa unaweza kuidhinishwa tu na baraza la usalama lenye wanachama 15, ambapo wanachama watano wa kudumu wana kura ya turufu. Mwezi uliopita, Marekani ilipiga kura ya turufu azimio la kutambuliwa kikamilifu kwa Palestina kama taifa.
Bila hata idhini ya Baraza la Usalama la uanachama kamili, bado Wapalestina watanufaika.
Baraza hilo litakapokutana mwezi Septemba, Palestina itakuwa na haki ya kuketi miongoni mwa nchi wanachama kwa mpangilio wa alfabeti. Palestina pia, itaweza kutoa taarifa kwa niaba ya kikundi, mapendekezo ya wafadhili, kupendekeza vipengele katika ajenda ya muda, na kuibua hoja za utaratibu.
Wapalestina hawatakuwa na kura ya Baraza Kuu, wala hawatoweza kuwasilisha ugombeaji kwa vyombo vikuu vya Umoja wa Mataifa kama vile baraza la usalama na Baraza la Kiuchumi na Kijamii.
Hata hivyo, makundi yanayoiunga mkono Israel yanahofia kwamba kura tofauti ya Baraza Kuu inaweza kuruhusu kuchaguliwa kwa Wapalestina kwenye Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa. Hili linaweza kuwa jukwaa ambapo ukiukaji wa haki za binadamu wa Israel unaweza kufunguliwa mashtaka.
Ni kipi kilichomo kwenye kura hiyo?
Nchi tisa zilizopiga dhidi ya Palestina kura dhidi ya uanachama wa Palestina ni pamoja na Marekani, Israeli, Argentina, Jamhuri ya Czech, Mikronesia, Nauru, Palau, Hungary, na Papua New Guinea wakati waliounga mkono uanachama wa Palestina ni Urusi, China, India, Indonesia, Afrika Kusini, Ufaransa, Hispania, Ubelgiji na nchi nyingine kadhaa za mashariki mwa Ulaya.
Licha ya Ujerumani kuiunga mkono Israeli kwa nguvu zote katika usambazaji wake wa silaha hatari, haikupiga kura, pamoja na Uingereza, Canada, Sweden na wengine 21.
Hata hivyo, hata kama Palestina itapata kutambuliwa kikamilifu katika Umoja wa Mataifa, hili halitobasilisha ukweli wowote uliopo. Mamlaka na eneo la Palestina hazimo kwenye ajenda ya kura hizi.
Katika kutetea kura yake ya hapana, Naibu Balozi wa Marekani Robert Wood alidai kuwa utaifa wa Palestina unaweza tu kutambuliwa kupitia matokeo ya mazungumzo ya moja kwa moja na Israeli.
Marekani na Israel zinatambua kikamilifu kwamba hakuna mazungumzo kama hayo yaliyo mezani. Na madai ya mazungumzo ni udanganyifu tu. Marekani imekuwa na miongo mitatu kuhakikisha mazungumzo yanafanyika. Badala yake, tawala mbalimbali zilishirikiana na Israeli zinapuuzia kwa makusudi mazungumzo haya.
Badala yake, Marekani iliizawadia Israeli kwa mauzo ya silaha na usaidizi wa kila mwaka. Wakiwa wamejihami na Marekani na mataifa mengine ya Magharibi, Israeli ilibadili hali halisi na kunyang'anya ardhi zaidi. Tangu mwaka 1967 hadi 2017, kulingana na Amnesty International, Israeli imenyakua ardhi ya hekta 100,000.
Zaidi ya maili za mraba 386 za wizi wa ardhi zimepunguza taifa la Palestina hadi chini ya robo ya kile kilichotengwa mwaka 1948. Mwaka 2024 hekta nyingine 800 za ardhi ya Palestina zilichukuliwa, na maili nyingine za mraba 3 za ardhi ziliibiwa.
Wakati wa upigaji kura wiki iliyopita, balozi wa Israeli Gilad Erdan, alilaani mataifa yote yaliyopiga kura kuunga mkono azimio hilo.
Aliuchana Mkataba wa Umoja wa Mataifa mbele ya wanachama wote kama kitendo cha kupinga. Erdan anaweza kutojali ukweli kwamba ni Mkataba uleule wa Umoja wa Mataifa ambao aliuvunjia heshima ndio ulioipa Israeli utaifa.
Cha kushangaza zaidi ni tuhuma za Erdan kuwa UN inakaribisha "taifa la ugaidi" katika Umoja wake . Iwapo kutakuwa na sababu ya ulimwengu kuelewa kwa nini hakuna amani katika eneo hilo, inaweza kutokana na mtazamo wa mwakilishi wa Israel katika Umoja wa Mataifa na shughuli za mauaji ya kimbari za Israeli kwa muda wa miezi saba iliyopita huko Gaza.
Hispania na Ireland, pamoja na mataifa mengine kadhaa ya Umoja wa Ulaya, yanapanga kuitambua Palestina kama taifa mnamo Mei 21, kulingana na mkuu wa sera za kigeni wa EU, Josep Borrell.
Shambulizi la Oktoba
Hamas iliamua kushambulia baada ya mazungumzo yote na Israeli kushindikana. Kitendo hiki kinaonekana kuwaamsha watu katika usemi wa "kuondoa ukoloni." Hili lilibadilisha ukweli wa mambo na kuleta dhulma ya kihistoria iliyofanywa kwa Wapalestina kwa hadhira ya kimataifa kwa njia ya picha.
Hii ni mantiki iliyotolewa na mwanamapinduzi mwanafikra kutoka Martinique, Frantz Fanon. Katika kazi yake kuu ya hatua ya mapinduzi, The Wretched of the Earth, Fanon aliandika kwamba "kuondoa ukoloni siku zote ni tukio la vurugu."
Pengine mwanafikra na mwanazuoni wa Kipalestina Edward Said hatokubali, lakini Hamas inaonekana kuwakilisha kizazi kipya cha wapiganaji wa upinzani.
Upinzani daima hauna usawa . Hamas ina alama za mchakato wa kweli wa kuondoa ukoloni ikiwa itafaulu, kulingana na Fanon. Israeli inatambua tishio halisi linaloletwa na Hamas kama mbadilishaji mchezo, na hivyo imejitolea katika maangamizi yake.
Kuondolewa kwa ukoloni kunahusisha haja ya kupinga uvamizi wa kikoloni ambao Mamlaka ya Palestina imewezesha na ambayo sasa imekuwa jiwe la kusagia shingoni mwake kwa miongo mitatu.
Fanon alirejea kifungu kwenye Biblia: "Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho (Mathayo: 2016)." Kwa mtazamo wa Fanon, wahusika wakuu hushiriki katika shindano la umwagaji damu ambapo wa mwisho husogea mbele.
Oktoba mwaka jana, aina tofauti sana na yenye nguvu ya upinzani ilidhihirika katika jukwaa la michezo la Palestina ambayo inaweza kuwa jaribio la kwanza na hatimaye kubadili ukweli halisi.
Bila shaka, itakuja kwa gharama kubwa ya maisha na dhabihu ya Wapalestina. Hata hivyo, Wapalestina wana chaguzi mbili: utumwa wa daima au kuondolewa kwa ukoloni, kama Fanon angesema. Katika kanuni ngumu kama hii ya maadili, kura za kiishara katika Umoja wa Mataifa zinaweza kufanikisha jambo fulani, lakini zifanye kidogo sana.
Ebrahim Moosa ni Profesa katika Shule ya Keough ya Mambo ya Ulimwenguni, katika Chuo Kikuu cha Notre Dame huko Indiana nchini Marekani.