Baada ya anguko la utawala wa Habre mwaka 1990, vikosi vilivyosalia Chad vilionesha nia ya kutaka kuliunganisha taifa na kuweka mikakati madhubuti itakayowapa matumaini watu wa Chad na kila mmoja ahisi amehusishwa katika uendeshaji wa nchi.
Chini ya utawala wa Marehemu Rais Idriss Deby Itno(aliyeuawa na vikosi vya uasi Aprili 2021 katika shambulio lililopangwa na Front pour l’Alternance et la Concorde au Tchad FACT), zoezi kama hilo la kusaka mfaka na mshikamano wa taifa pia liliombwa na wapinzani. Hatahivyo badala ya kufanya mazungumzo na wapinzani wake, Marehemu Rais Idriss Deby alichagua kufanyika kwa majukwaa ya majadiliano mwaka wa 2018 na 2020; jambo ambalo wapinzani walisusia kushiriki.
Kuondoka kwa Idriss Deby sasa kumetoa fursa nyingine kwa wahusika kuketi na kuzungumza. Doha inasimama kidete cha raia wa Chad ikiwa na madhumuni ya kusaka mwafaka na mshikamano kupitia njia ya mazungumzo ya kina yatakayowahusisha washikadau wote muhimu. Tangu kuanza kwa mchakato wa mazungumzo hayo mnamo Machi 13, 2022 makubaliano ya Amani yaliafikiwa Agosti 8, 2022 na utiaji saini kati ya Jeshi na Kamati ya mpito kufanyika. Walioshuhudia utiaji saini wa makubaliano hayo ni wakiwemo; Mkuu wan nchi Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno, Rais wa Baraza la Kijeshi la mpito.
Kati ya washirikishwa wote 52(Kundi kutoka Roma, Kundi la Doha na Kundi maalum la Qatar) waliofanikisha mazungumzo, 43 waliridhia kutia saini kuonesha kuridhishwa na makubaliano huku 19 wakihisi makubaliano hayakukidhi vigezo vya mazungumzo. Walitaka hakikisho la awali kutoka kwa Rais wa Baraza la Kijeshi la mpito kuwa atakabidhi madaraka kwa raia na kumtaka kutogombea urais katika siku za usoni.
Hatahivyo wapo waliohisi kuwa wasiwasi huo unaweza ukashughulikiwa nje ya makubaliano hayo kwani tafsiri yake inahitaji kufafanuliwa zaidi kupitia mchakato wa mahakama.
Kurejea kwa Mahamat Deby Itno nchini Chad akitokea Doha kulipokelewa kwa mbwembwe na vifijo, raia wengi wakihisi utiaji saini wa makubaliano hayo ya amani ni mwanzo mpya wa kuijenga Chad na kuamua mustakabali wake.