Na Claire Taylor
Mnamo Februari 10, msanii aliyeshinda tuzo na msanii maarufu wa hip-hop AKA - mzaliwa wa Kiernan Forbes - alipigwa risasi nje ya mkahawa huko Durban.
Mauaji haya ya hali ya juu yalirudisha uangalizi kwenye virusi vya unyanyasaji wa bunduki unaoua watu 30 kila siku nchini Afrika Kusini.
Hatu zilizochukuliwa kufuatia kifo cha AKA zimelenga kuwakamata wahusika. Ingawa kupata haki ni muhimu, hasa kwa familia yake na marafiki ili kuleta faraja, mambo mengine kama vile jinsia, matumizi ya silaha na yanapaswa kujadiliwa ikiwa tunataka kulinda watu dhidi ya uhalifu wa mauaji, hasa ya risasi.
Jinsia na uhalifu
Uhalifu na unyanyasaji nchini Afrika Kusini hutofautiana kulingana na jinsia ya mwathirika. Wanaume na wanawake hupitia hali hii kwa njia tofauti.
Wanaume, kama AKA, ndio waathirika wengi wa uhalifu - wahanga 63 kati ya 73 wa mauaji nchini Afrika Kusini kwa siku ni wanaume.
Ingawa wanawake wana uwezekano mdogo wa kuuawa, wako katika hatari kubwa ya kuuawa majumbani mwao na wapenzi wao wa karibu na pia wako katika hatari kubwa ya unyanyasaji wa kijinsia.
Bila kujali jinsia ya mwathirika, karibu kila wakati mhalifu ni mwanaume. Ili kuelewa ni nini kinachowasukuma wanaume kufanya vurugu, ni muhimu kuvunja uhusiano kati ya ubabe wa kiume na ukatili.
Kwa mfano, utafiti uliochapishwa katika Jarida la Sheria ya Jinai na Sayansi ya Uhalifu mnamo 1987, ulithibitisha uhusiano wa karibu kati ya kuwa mhalifu na hali ya kuonewa.
Hii inaangazia uwezekano mkubwa wa wanaume kuwa wahanga wa unyanyasaji na umuhimu wa kuwalinda wanaume (na wavulana) ili kuondokana na mzunguko huu wa ukatili.
Kupunguza matumizi ya bunduki
Bunduki ni chombo kilichotengengezwa kwa nia ya kuua, na kadiri bunduki zinavyopatikana, ndivyo watu wanavyopigwa risasi na kuuawa, kujeruhiwa au kutishiwa.
Hivyo, kupunguza upatikanaji wa bunduki huokoa maisha, kama uzoefu wa Afrika Kusini unavyoonyesha. Kadiri idadi ya bunduki ilivyopungua mapema miaka ya 2000 kutokana na kupitishwa Sheria ya Kudhibiti Silaha (2000), ndivyo pia kiwango cha vifo vya risasi nchini Afrika Kusini kilivyopungua.
Utafiti uliofanywa na Richard Matzopoulos na kuchapishwa katika Jarida la Marekani la Afya ya Umma unaonyesha kwamba maisha ya watu 4,500 yaliokolewa baada ya kuchukuliwa hatua za kupunguza matumizi ya bunduki katika miji mitano ya Afrika Kusini kati ya 2001 na 2005.
Hata hivyo, wakati idadi ya bunduki nchini Afrika Kusini ikiongezeka kwa kasi kuanizia mwaka 2010/11 kutokana na kulegea kwa hatua za udhibiti wa silaha kulikosababishwa na uhaba wa bajeti, mipango duni na uhalifu unaohusisha ulaghai, rushwa na wizi, vurugu za matumizi ya bunduki zimeongezeka kwa kasi pia.
Kufikia 2022, idadi ya watu waliopigwa risasi na kuuawa ilikuwa inakaribia ile ya 1998, ambapo watu 34 walipigwa risasi kila siku.
Ulimwenguni kote, utafiti umegundua kuwa kupunguza idadi ya bunduki huokoa maisha. Moja ya uzoefu muhimu ni ule wa Colombia na Vecino-Ortiza et al mnamo 2020.
Hii inaonyesha kwamba kupiga marufuku watu kubeba bunduki hadharani katika miji ya Bogotá na Medellín kuliokoa maisha ya watu 30 kila mwezi, na kwamba maisha zaidi 45 yangeweza kuokolewa kila mwezi ikiwa vikwazo sawa na hivyo
Hatua gani zichukuliwe?
Kulingana na takwimu za kitaifa za uhalifu nchini Afrika Kusini, mauaji mengi hayahusiani na uhalifu bali ni matokeo ya mabishano na kutoelewana.
Moja ni kauli iliyozoeleka ya kutaka askari polisi nchini Afrika Kusini waongezwe zaidi ili waweze kukabiliana na uhalifu. Hata hivyo, hii haiwezi kuleta matokeo makubwa.
Badala ya kutaka vikosi vya polisi zaidi, ni vema nguvu kubwa itumike kuchunguza na kuelewa chanzo cha uhalifu na mauaji.
Pili, ni hoja ya kejeli na hatari kwamba raia wenye silaha husababisha jamii kuwa salama bila kujali ukweli kwamba uwepo wa silaha mtaani huongeza hatari hasa pale mabishano yanapoibuka na kupelekea mauaji.
Kupunguza ghasia na uhalifu nchini Afrika Kusini si jambo la moja kwa moja, lakini uingiliaji kati lazima uwe wa msingi wa ushahidi, na uzingatie athari za jinsia, silaha na makusudi.
Moja ya hatua za ufanisi zaidi ni kupunguza upatikanaji wa bunduki. Ingawa huduma ya polisi haiwezi kufuatilia ipasavyo migogoro baina ya watu, ina jukumu muhimu katika kurejesha na kuharibu mkusanyiko wa silaha nchini humo, hasa silaha haramu.
Hata hivyo, juhudi za kugeuza hali hii zitaleta ufanisi ikiwa tu tutafunga bomba linazovujisha bunduki haramu ndani ya jamii zetu. Bomba kubwa zaidi ni bunduki halali zinazomilikiwa na Serikali na raia, huku raia wakiripoti upotezaji au wizi wa wastani wa bunduki 24 kila siku.
Hii ina maana kwamba inabidi tuimarishe kwa haraka udhibiti wa bunduki na risasi halali ili kuzuia kuvuja kwenye bwawa hilo haramu. Mauaji ya AKA yawe mstari uliochorwa mchangani utakaosukumwa hatua za kukomesha mauaji ya risasi nchini Afrika Kusini.
Mwandishi, Claire Taylor, ni mtafiti katika Shirika lisilo la Kiserikali la Gun Free South Africa (GFSA), linalofanya kampeni dhidi ya matumizi mabaya ya silaha.
Angalizo: Maoni yaliyotolewa na mwandishi sio lazima yaakisi mtazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.