Afrika yahitaji majibu ya makosa wakati wa Uviko-19

Afrika yahitaji majibu ya makosa wakati wa Uviko-19

Ni muhimu kufanya utafiti wa kina, ili kosa kama hilo lisijirudie.
Ukilinganisha na mabara mengine, Afrika ilikuwa na vifo vichache kutokana na janga na Uviko-19./Picha: Reuters

Na Toby Green

Miaka minne imepita tangu Shirika la Afya duniani (WHO) kuutangaza ugonjwa wa Uviko-19 kama janga la kimataifa.

Pia ni kumbukumbu muhimu tangu la Afrika kuchukua hatua za kukabiliana na janga hili, kama vile uamuzi wa Rwanda kutoruhusu ndege kutoka China kutua nchini humo, mnamo Januari 31, 2020.

Katika kukabiliana na maradhi haya, wachambuzi tofauti walirejelea uzoefu wa Guinea, Liberia na Sierra Leone na namna walivyopambana na changamoto za Ebola kati ya mwaka 2014 na 2015, wakisisitiza kama kiashiria kizuri cha kukabiliana na magonjwa mengine ya milipuko.

Hata hivyo, kadiri muda unavyozidi kwenda ndivyo inavyoonekana dhahiri makosa yaliyofanywa na jumuiya za kimataifa kutokana na maradhi hayo hatarishi. Kimsingi, Uviko-19 lilikuwa ni janga kwa bara la Afrika.

Wakati uchunguzi wa kina kuhusu ugonjwa huu ukiendelea nchini Uingereza, ni wakati muafaka jambo kama hilo kufanyika barani humu ili makosa yaliyosababishwa na mataifa tajiri yasijirudie.

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa idadi ndogo ya vifo vilivyoripotiwa barani Afrika ni ishara tosha ya namna bara la Afrika liliweza kukabiliana na janga hili. Hata hivyo, hii sio namna sahihi ya kuangalia jambo hili.

Funzo kutoka Ebola

Ikiwa na wastani wa umri wa chini ya miaka 20, ilikuwa ni lazima kwa bara la Afrika kuwa na vifo vichache kutokana na Uviko-19. Hii si dalili ya mafanikio ila zahma iliyokumbana nayo kwa kujiaminisha kuwa madhara ya ugonjwa huo yalikuwa sawa wa pande zote.

Kosa la kwanza lilikuja na zuio la safari za nje ya nchi. Katazo hili lililetwa na WHO, ambao baada ya uchunguzi wao katika mji wa Wuhan, Februari 25, 2020, walikuja na pendekezo la kufunga anga.

Hata hivyo, mifano kama hiyo ilijaribiwa katika miji ya Freetown na Monrovia, wakati wa janga la Ebola.

Hata madaktari wasio na mipaka walipinga hatua hii wakisisitiza umuhimu wa kuimarisha uchumi wa nchi nyingi za bara la Afrika.

Ni vyema kwa WHO kufahamu tafiti za aina hii, ingawa hata wao wenyewe walishauri vivyo hivyo.

Kosa la pili ilikuwa ni kudharau dhana ya idadi ya watu. Kufikia mwisho wa mwezi wa tatu, wachambuzi walituaminisha kuwa kwa kuzingatia suala la umri, ugonjwa huo usingekuwa hatari kubwa kwa bara la Afrika.

Ufinyu wa Nafasi

Utafiti huu ulipuuzwa, kwa ajili ya mkakati wa kutokomeza ambao haungeweza kufanikiwa katika nchi ambazo makazi yasiyo rasmi yalichochea kuenea kwa kasi kwa maradhi ya Uviko-19.

Kisha likaja kosa la utekelezaji wa amri ya kutotoka nje na kuwafanya watu kurundikana sehemu moja, hasa sehemu zisizo rasmi kama Nairobi, Lagos na Kinshasa.

Kuenea kwa kasi kwa ugonjwa huu kulisababiswa na watu kukaa ndani na kwenye sehemu finyu na hivyo kuongeza maambukizi ya Uviko-19.

Na hii ilitokana na ukweli kwamba wanasayansi wengi kutoka WHO na mataifa mengine makubwa duniani wanatokea mataifa tajiri. Cha kushangaza, ni kwamba wataalamu hao hakuwa na uelewa wa tabia za maisha ya kijamii kwenye miji mingi barani Afrika.

Hatua hii inaakisi sera za kikoloni na utegemezi wa kiuchumi wa taasisi nyingi za Kiafrika kwa wafadhili kutoka nchi za magharibi na China. Hata hivyo, uchunguzi huu haupaswi kuegema kwenye masuala ya kisayansi.

Kosa la nne lilikuwa ni kudharau viashiria vya kijamii katika masuala ya afya yenye kuzingatia muktadha wa kijamii.

Udhaifu wa mifumo ya afya

Kwa muda mrefu, wanasayansi wa kijamii wametambua uhusiano wa karibu katika ya afya na mali. Katika nchi nyingi za kimasikini, uhusiano kati ya pato la taifa na umri wa kuishi zimefafanuliwa kwenye “Prescott curve”.

Kama ambavyo pato la taifa huongeza umri wa kuishi, ndivyo itavyoweza kupunguza. Kufungwa kwa masoko yasiyo rasmi, usafiri na amri za kutotoka zilikuwa ni sera zilizoongeza umasiki barani Afrika. Sera hii ililenga zaidi kupunguza utajiri, kufifisha afya na umri wa kuishi barani Afrika.

Wakati Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) likisema kuwa zaidi ya nusu ya watu wanaokabiliwa na njaa kali waliingia katika hali hiyo kuanzia mwaka 2020, na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP) likidai kuwa takribani Waafrika milioni 50 walipitia umasikini wa kutupwa wakati wa janga la Uviko-19, ni wazi kuwa sera za WHO zilififisha huduma za afya barani Afrika.

Na zaidi hayo, bado kuna masuala yanayopaswa kupewa msisitizo. Kwanza kabisa ni kufungwa kwa shule na kuzuka kwa ajira kwa watoto. Pili, ni namna ambavyo amri za kuzuia watu kutoka zimesababisha kukosekana kwa uendelevu wa shughuli za kiuchumi.

Tatu, ni namna kivuli cha janga hili kulivyochochea ukatili wa kijinsia majumbani, na nne ni athari za kusitishwa kwa huduma za usafiri duniani kwenye usambazaji wa madawa ya Malaria na vipimo vingine muhimu.

Hata hivyo, mchakato wa kuanzisha uchunguzi huu utaishia njiani. Jambo moja pekee liko wazi: yeyote anayeiendesha, haiwezi kuwa WHO au taasisi nyingine yoyote ya kimataifa ambayo inashangilia kuwekwa kwa sera hizo mbovu katika bara.

TRT Afrika