Huku mwezi wa Agosti ukimalizika taratibu, msimu wa tuzo za muziki kwa mwaka 2023-2024 unanza kukaribia na uteuzi wa tuzo kwa jukwaa mbalimbali za burudani unazidi kuwa kwenye vichwa vya habari.
Trace Music, jukwaa la muziki la kidijitali la Afrika nzima, limezindua orodha ya wateuliwa kwa tuzo zake za kwanza za muziki barani Afrika, zinazotarajiwa kufanyika Kigali, Rwanda, tarehe 21 Oktoba, 2023.
Jumla ya tuzo ishirini na mbili zinapatikana, na uteuzi unajumuisha wasanii wanaouza vizuri kwenye zaidi ya nchi 30 barani Afrika, Amerika Kusini, Karibiani, Bahari ya Hindi, na Ulaya.
Katika kipengele cha msanii bora wa kiume wa Kiafrika, Nigeria ina uwakilishi imara kutoka kwa wasanii kama Asake, Burna Boy, Davido, na Rema.
Hata hivyo, ushindani mkali utatokea kutoka kwa Diamond Platnumz (Tanzania), Didi B (Ivory Coast), na K.O. (Afrika Kusini).
Kwenye kipengele cha msanii bora wa kike wa Kiafrika, Ayra Starr (Nigeria), Josey (Ivory Coast), na Nadia Mukami (Kenya), Soraia Ramos (Cape Verde), Tiwa Savage (Nigeria) na Viviane Chidid (Senegal) wote watapambana kushika nafasi ya juu.
Pambano gumu zaidi litakuwa, hata hivyo, katika kitengo cha wimbo wa mwaka, ambapo nyimbo 12 zimeorodheshwa kwenye kipengele hicho yenye ushindani mkubwa.
"Wimbo wa Last Last" kutoka kwa mshindi wa Grammy, Burna Boy, umeteuliwa kwa tuzo, lakini unapaswa kushindana na ushindani mkali, hususan kutoka kwa "Calm Down" - Rema (Nigeria), "Sugarcane" - Camidoh (Ghana), "Peru" - Fireboy DML (Nigeria) pamoja na Ed Sheeran (UK), "BKBN" - Soraia Ramos (Cape Verde), "Encre" - Emma’a (Gabon), "Cough" - Kizz Daniel (Nigeria) na "Rush" - Ayra Starr (Nigeria) miongoni mwa wengine.
Cameroon inakuja kwa nguvu kwenye kundi hilo, na waimbaji wawili, Krys M. na Libianca, wamechaguliwa kwenye kipengele cha wasanii chipukizi bora.
Washindi wa vipengele mbalimbali watakabidhiwa tuzo za Trace Awards, ambazo ni kazi za sanaa za kipekee zilizoundwa na mchongaji na mbunifu maarufu kutoka Kongo, Dora Prevost.
Tuzo za muziki za Kiafrika zimekuwa zikicheza jukumu muhimu katika kuangazia wasanii katika bara hilo na kusaidia kuonyesha ubora na tofauti ya muziki wenye msingi wa Kiafrika katika miziki kama Afrobeat, Dancehall, Hip Hop, Afro-pop, Mbalax, Amapiano, Zouk, na Kizomba, kati ya mingine.