Broad Masingisa: Nimejifunza kuandaa filamu mtandaoni

Broad Masingisa: Nimejifunza kuandaa filamu mtandaoni

Kilichonisukuma kuingia kwenye fimau ni upotoshaji juu ya mila za kimasai
Broad Masingisa anasema kutumbukia kwake katika tasnia ya filamu hapo awali kuliibua lawama kutoka kwa jamii yake. Picha \ TRT Afrika

Broad Masingisa aliinga rasmi kwenye uandaaji wa filamu mwaka 2018 akiwa hana mafunzo yoyote bali shauku ya kutaka kubadili taswira ya namna baadhi ya mambo kuhusu mila za kimasai yanavyoelezwa.

Masingisa ambaye ni mkazi wa mkoa wa Morogoro toka jamii ya wamaasai amekua akishuhudia mapigano baina ya wakulima na wafugaji mara kwa mara, jambo ambalo limewaacha baadhi ya jamaa zake na majeraha ya kudumu kitu ambacho kilimfanya aone iko haja ya kutumia filamu kwa lugha ya kimasai na Kiswahili kuwaelimisha juu ya mambo mbalimbali ukiwemo upendo kati yao na majirani zao wakulima lakini kuzikataa na kuachana na mila za kandamizi zilizopitwa na wakati.

Filamu za Broad Masingisa zimempatia tuzo na kutambulika nchini Tanzania. Picha \ TRT Afrika

Muandaaji huyu wa filamu hajaenda shule lakini amekua akitizama fimu za wengine kujifunza “nimekuwa niangalia filamu za wengine za nje na ndani lengo kujifunza wanavyoandika stori na namna walivyo andaa filamu zao” Masingisa anasema anaweza kurudia kutazama filamu mora zaidi ya mara tano ili kuielewa kiundani lakini zaidi kuelewa mbini za uandaaji ambazo waandaaji wametumia.

Mwishoni mwa mwake 2018 ikiwa ndio ulikua mwaka wake wa kwanza kwenye filamu Masingisa alilazimika kuanchana filamu ambayo ilikua kwenye hatua za mwisho za uandaaji sababu ya kukosa ubora, Filamu hiyo iliyokuwa na jina la time for maasai (Ni muda wa wamasai) ilikua na ubora mdogo hasa kwenye picha na sauti kutokana na kutumia vifaa duni na kutokua na uelewa mzuri wa kupangilia matukio.

Jambo hili lilimvunja moyo na hata jamii kuona ni kama anapoteza mud ana asingefanikiwa kutokana na kutokua na elimu yoyote ya filamu.

Broad Masingisa anapata njama za filamu zake kutokana na uzoefu wake wa kitamaduni kama Mmasai. Picha \ TRT Afrika

Lakini licha ya kupoteza fedha na muda hakukata tamaa aliendelea mbele na sasa filamu yake ya Gisoi ambayo iliingia pia kwenye Tuzo za filamu Tanzania ndio filamu bora kwa mkoa wa Morogoro kwenye kipengele cha mavazi ya kitamaduni lakini pia kwenye kipengele cha filmu bora yenye maudhui ya kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa Watoto na wanawake.

Kwa mujibu wa masingisa jamii ya waasai imekua ikichukulia filamu kama uhuni hivyo kupewa nafasi ndogo jambo ambalo anatamani kuona likibadilika kiwani ana amini filamu ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na nimuhimu vijana wa jamii yake watumie vipawa vyao kuelimisha jamii kupitia filamu kwani ni njia rahisi ya kufikisha elimu.

Mfano filamu yake ya Gisoi inayozungumzia mtoto kuvalishwa pete akiwa tumboni, ambapo mwanaume humvalisha mama mjamzito bangili na iwapo mtoto atakaye zaliwa ni wa kike basi atakua mke wake jambo linalo mnyima uhuru mtoto wa kike kuchagua mwenza lakini uhuru wa kujiendeleza kimaisha ikiwa ni pamoja na kupata elimu.

Broad Masingisa ana matumaini kuhusu uwezo wa filamu kubadilisha mitazamo miongoni mwa Wamasai. Picha \ TRT Afrika

Pamoja na kutumia mitandao ya kijamii zaidi kujifunza pia anashirki kwenye semina mbalimbali zinazo andaliwa na mabaraza ya Sanaa ili kujifunza zaidi juu ya maadili na miiko ya tasnia hiyo hapa nchini Tanzania.

Siku za hivi karibuni alipata nafasi ya kushiriki kwenye filamu fupi iliyoandaliwa na kampuni kutoka nchini china iliyolenga kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii lakini pia kuonesha ushirikiano na urafiki wa muda mrefu kati ya china na Tanzania ambapo pia raisi wa Tanzania Daktrari Samia Suluhu Hassan alishiriki.

Broad Masingisa anasema kutumbukia kwake katika tasnia ya filamu hapo awali kuliibua lawama kutoka kwa jamii yake. Picha \ TRT Afrika

Ukiachana na kaze zake za filamu pia kijana huyu wa kimasaai amekua akiandaa matamasha mbalimbali kupinga na kukemea mila potofu lakini pia amekua akindaa makala mbalimbali zinazolenga kuhifadhi matukio ya kimila ambayo ni chanya na angetamani kizazi kimoja hadi kingine kirithishane utamaduni huo.

TRT Afrika