Na Imran Khalid
Kwa mara nyingine tena, eneo la mashariki ya Kati limejikuta kwenye mvutano wa kisiasa wa kijiografia huku mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora ya Iran dhidi ya Israel yakipeleka mshtuko katika eneo hilo.
Kulipiza kisasi kwa Iran, kumechochewa na shambulio la Israeli lililolenga jengo la ubalozi wa Iran nchini Syria, hii ni alama ya vita vya moja kwa moja kati ya nchi hizo mbili na sio vita vya kupitia wakala, kama ilivyokuwa hapo mbeleni.
Badala ya kutumia mbinu za awali za vita vya siri vya wakala; Iran imeishambulia Israeli moja kwa moja kutoka katika ardhi yake, hatua ya kushangaza na ya uchochezi.
Hata hivyo, ushujaa huu unaonekana kama vitisho tu na sio shambulio la kikweli.
Kufuatia shambulio la Israel nchini Syria ambalo liligharimu maisha ya makamanda saba wa Iran akiwemo Brigedia Jenerali Mohammed Reza Zahedi, kulipiza kisasi kwa Tehran kunaonekana kama maonyesho ya nguvu yaliyofanywa kwa umakini na sio kuwa ni uchochezi wa vita.
Licha ya maneno makali kati ya nchii hizo mbili, dalili za utulivo zinaonekana kuwa karibu.
Taarifa ya Iran kwa Umoja wa Mataifa mara tu baada ya shambulio lake la kulipiza kisasi kwamba suala hilo linapaswa kuzingatiwa sasa "limekamilika", pamoja na kufunguliwa kwa anga na mataifa jirani, limeonyehsa ishara ya kupunguza makali ya vita.
Hata hivyo, maonyesho ya hivi majuzi ya Iran ya "uchokozi hafifu" yamechohchea baadhi ya vichwa sugu wa Israeli kutaka kulipiza kisasi wa nguvu.
Ingawa Tel Aviv imeahidi kulipiza kisasi dhidi ya shambulio la hivi la Iran, mpango wake bado haujuikani. Badala ya kulipiza kisasi, Israeli huenda ikapunguza makali ya kulipiza kisasi na kuepuka makubaliono ya wazi - kwa sababu ya upinzani mkubwa kutoka kwa Washington na miji mikuu mingine ya Magharibi, ambayo haiwezi kumudu vita vya hali ya juu katika Mashariki ya Kati wakati ambapo moto wa vita vya Ukraine bado unaendelea.
Chaguo la kupunguza ya makali ya vita linaonekana kuwa chaguo lisilo hatari sana, kuruhusu Israeli kuzidisha vita vyake vya siri huku ikiepuka makabiliano ya moja kwa moja.
Wakati Biden amethibitisha uungaji mkono usioyumba wa serikali yake kwa usalama wa Israel, pia ameashiria kusitasita kushiriki katika operesheni ya kukera dhidi ya Iran.
Hii inaiweka Israel katika hali ngumu ambapo inabidi kusawazisha hamu yake ya kulipiza kisasi huku ikiepuka hatua yoyote inayoweza kuzua mzozo mpana zaidi.
Wakati huo huo, Iran pia imepeperusha bendera nyeupe. Iran imedokeza kuwa mashambulizi yake dhidi ya Israel yameisha kwa sasa. "Suala hilo linaweza kufungwa," ujumbe wa Iran kwenye Umoja wa Mataifa ulisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Hii inaangazia changamano na ugumu katika masuala ya utawala na nguvu Mashariki ya Kati, ambapo mara nyingi uchochezi na ubabe hufichwa na mahesabu ya kina.
Vita kwa ajili ya utawala wa kikanda
Katika mazingira haya tete, kila hatua hulemewa na matokeo na madhara yake. Mpambano wa hivi majuzi kati ya Iran na Israeli ni sura tu katika sakata la muda mrefu la ushindani wao tata.
Ongezeko wa hali tata wa hivi karibuni, likionekana kuwa mwendelezo wa mivutano wa kikanda na mzozo unaoendelea Gaza, ila ukweli ni: vita vya utawala katika Mashariki ya Kati.
Kiini cha mzozo huu ni mapambano ya zamani ya madaraka na ushawishi, huku Iran na Israeli zikigombea ukuu katika eneo lililojaa ukosefu wa utulivu. Kuchukia kwao kwa pamoja mataifa ya Kiarabu kumezua muungano wa nchi hizo mbili, uliodhihirika katika ushirikiano wao wa kimyakimya kufuatia uvamizi wa Marekani wa 2003 nchini Iraq.
Wakati huu muhimu ulibadilisha sura ya eneo, na kuipa Israeli nguvu ya nyuklia huku ikiimarisha nguvu ya Iran juu ya Baghdad. Hata hivyo, hali ya ushirikiano hufunika tofauti za kimsingi za maslahi.
Kwa Israeli, kudumisha ubambe wake wa nyuklia ni jambo la msingi, na kuendesha juhudi za kukandamiza matarajio ya nyuklia ya Iran kwa gharama yoyote. Kinyume chake, Iran inaziona silaha za nyuklia kama hitaji la kimkakati.
Mvutano unapozidi kupamba moto na ndege zisizo na rubani zikijaa angani, Mashariki ya Kati kwa hakika inaelekea kwenye ukingo wa hatari, ambapo jitihada za kutaka ukuu zinatishia kulitumbukiza eneo hilo katika machafuko.
Katika mchakato huu wa hali ya juu wa siasa za madaraka, hakuna atakayekukubali kushindwa. Kwa Iran, kuhifadhi miundombinu yake ya nyuklia itakuwa na kipaumbele.
Ndio maana licha ya kurusha makombora, lakini Iran inafahamu kwa kina matokeo mabaya ya makabiliano ya moja kwa moja na Israel, ndio sababu inaenda mwendo wa tahadhari ili kuepuka kutoa kisingizio cha kuingilia kijeshi. Iran ilifanya kwa uangalifu shambulio hili dhaifu ili kuepusha uharibifu wowote wa raia au wa kijeshi ili kuzuia uwezekano wa athari yoyote ya haraka na kali kutoka kwa Israeli, ambayo ingeweza kuzidisha hali hiyo.
Uhifadhi wa vifaa vyake vya nyuklia, ni muhimu kwa matarajio yake ya muda mrefu, kwa hivyo ni wazi mno kufahamu ulipizaji wa kisasi uliyofanywa kwa makini sana ili kupunguza makali ya vita.
Zaidi ya hayo, Tehran inafahamu ulazima wa kujihusisha na ujanja wa kidiplomasia, pamoja na kuzingatia majadiliano ya faragha yanayoendelea na serikali ya Rais wa Marekani Joe Biden.
Matarajio ya kurejea kwa makubaliano ya nyuklia ya 2015 inategemea sana kudumisha kiwango cha utulivu katika eneo hilo, kwani kuongezeka kwa hali yoyote ya mvutano kunaweza kuhatarisha juhudi zinazoendelea za kidiplomasia.
Katikati ya matatizo haya, Iran inatembea kwenye njia hatari, ikitambua tishio lililopo la kuingilia kati kwa Marekani kumtetea mshirika wake wa Israel. Iran inajikuta katika hali ya hatari na tata, huku akijifanya mkaidi na vile vile kufahamu ukweli wa umniyano wa nguvu ya kijografia katika eneo.
Licha ya vitisho vyake, Tehran inafahamu vyema matokeo ya kujihusisha na makabiliano ya kijeshi ya moja kwa moja na nguvu ya pamoja ya Marekani na Israel.
Njia yake ya mashambulio inaongozwa zaidi na tahadhari, utawala wa Irani unaelewa athari zinazowezekana kutokezea kwenye mashambulio hayo, pamoja na kuzingatia maonyo ya serikali ya Biden.
Zaidi ya hayo, hesabu za Iran zinapita zaidi ya uwezo wa kijeshi tu, huku zikizingatia mienendo ya kisiasa ya kijiografia.
Kuwa makini na hisia za kimataifa, haswa kuhusu vitendo vya Israeli huko Gaza, inaashiria ujanja wa kidiplomasia wa Tehran ili kupata kuunga mkono kwa kulipiza kisasi kwake.
Hatimaye, hesabu za kimkakati za Tehran zinazunguka katika kuhifadhi maslahi yake huku zikizingatia kubadilika kwa siasa za kikanda.
Katika hali tete iliyojaa masuali, tahadhari inaibuka kwa waendehsaji siasa za Iran. Mienendo inayozunguka chokochoko za mashambulizi ya Iran zinaonyesha mwingiliano tata wa nguvu wa kikanda.
Urusi na Uchina, kwa kuzingatia masilahi yao ya kimkakati, zimewasilisha ujumbe wazi kwa Tehran: hatari za migogoro ya moja kwa moja ni kubwa kuliko faida yoyote inayoweza kupatikana. Kwa kuangalia kwa makini matakwa yao ya kiuchumi na kimkakati, madola hayo mawili yanaonyesha kusitasita kwa matarajio yoyote ya kupamba moto zaidi kwa mzozo wa Iran na Israel. Kiini cha hesabu zao ni hamu ya kulinda masilahi yao ya pande zote katika Mashariki ya Kati.
Kusita kwao kuingizwa katika moto wa kimataifa ni kizuizi kilichohesabiwa kinacholenga kulinda maslahi yao ya kiuchumi na kijiografia.
Hata hivyo, katikati ya mchakato wa maslahi yanayoshindana na miungano inayobadilika, hali ya mzozo inajitokeza sana, ikitoa ishara ya kutokuwa na uhakika juu ya mazingira tete ya siasa za kijiografia za Mashariki ya Kati. Katika kinyangariko hiki, ni ngumu sana kukosea.