Jumuiya ya Ulaya imesisitiza kuwa simu zote na vifaa vingine vidogo lazima viendane na nyaya za kuchaji za aina ya USB-C kuanzia mwisho wa mwaka ujao, hatua ambayo inasema itapunguza taka na kuwaokolea pesa watumiaji.
Kwa muda mrefu, kampuni hiyo ilikuwa imejitetea kuwa nyaya zake zilikuwa salama zaidi kuliko chaja za USB-C, ambazo tayari zimetumika na Apple kwenye vifaa vingine na hutumiwa sana na washindani wake ikiwa ni pamoja na Samsung, mtengenezaji mkubwa wa simu za mkono duniani.
"USB-C imekuwa kiwango kinachokubalika ulimwenguni. Kwa hivyo tunaleta USB-C kwa iPhone 15, " alisema Kaiann Drance, makamu wa Rais wa apple wa mauzo wa iPhone kwenye hafla ya uzinduzi.
Kamishna wa umoja wa ulaya Thierry Breton aliijibu iPhone kubadili kiunganishi kipya kwa kusema chaja za ulimwengu ni "hali ya kawaida."
Soko la bara Ulaya "liko huru, lakini kwa masharti yetu," Breton alisema katika taarifa iliyotolewa.
Mabadiliko ya Apple yanakuja wakati makampuni makubwa ya Teknolojia katika eneo la Silicon Valley yanazidi kukabiliwa na kupungua kwa mauzo ya iPhones, na bei zake zinasukuma wateja kuchelewesha kuchukua toleo jipya ya simu za Iphone.
Kampuni hiyo pia imejikuta kwenye msukosuko wa kidiplomasia kati ya Marekani na China, huku ripoti zikisema kuwa serikali ya kikomunisti imewazuia watumishi wa umma kutumia simu zake za Apple.
"Apple ilihitaji kutoa zaidi ya badiliko ndogo tu ili kuleta tabasamu kwa watu juu ya kununua toleo jipya," mchambuzi wa Techsponential avi Greengart alisema pembeni mwa eneo la hafla hiyo ya uzinduzi.
"Nadhani walifanikiwa kwa hilo kwa upande wa mabadiliko, baadhi yao si machache mno."
Pamoja na maboresho ya kamera za iPhone na chips, Apple ilisema kuwa iPhone 15, ambayo inatoa aina nne za 15 (pichani), itakuwa na vifaa vya ndani ambavyo vinarahisisha ukarabati na muonekano mpya ambao unaruhusu kioo cha nyuma kubadilishwa kwa urahisi.
Urahisi kwa ukarabati ni mabadiliko yasiyotarajiwa na wateja wa awali.
Kujitofautisha na wengine
Mwezi uliopita, Apple ilisema kuunga mkono kupitishwa kwa sheria ya California iliyohitaji watengenezaji wakuu wa vifaa kuwawezesha watu kurekebisha vifaa vyao wenyewe bila kuvirudisha kwa kampuni.
Aidha, katika hatua ya kushangaza, Apple ilisema iPhone 15 Pro itakuwa $999 ambayo ni bei sawa na mtangulizi wake - Iphone 14 Pro Max; iPhone 15 Pro Max itaanzia $1,199 ongezeko la dola $100.
Apple pia ilizindua aina mpya ya saa ya Apple yenye uwezo wa kupokea na kukata simu au kazi zingine muhimu kwa njia ya kidole gumba.
Ukarabati rahisi
Kama kampuni nyingine yoyote, Apple ingependa kujivunia juu ya huduma mpya zenye kung'aa tofauti na sehemu mpya ya kuchaji.
Lakini wadadisi wengi walikubaliana kwamba kubadili USB - C ndio habari kubwa.
Watungaji sera wa EU wameeleza sheria hiyo itarahisisha maisha ya wenyeji wa Ulaya na kuondoa vikwazo vya chaja za kizamani.
Ili kufanya mpito iwe rahisi, Apple pia ilitoa nyaya mpya, pamoja na Adapta aina ya USB-C kwenye Umeme.
"Watumiaji wa kawaida wataghadhabishwa kwamba wanapaswa kubadilisha nyaya zao, lakini sidhani kama hiyo itaathiri mauzo," mchambuzi Greengart alisema.
"Yeyote mwenye vifaa vingi vya teknolojia tayari ana USB -C kila mahali."
Kushuka kwa biashara ya kampuni ya Apple
Katika robo ya mwaka iliyokamilika hivi karibuni, Apple ilishuhudia kushuka kwa mauzo ya iPhone kwa asilimia 2.4, ambayo ni sawa na takriban nusu ya mapato yote.
Soko lilionekana kutovutiwa sana na tangazo la Apple na hisa zilipungua kwa asilimia 1.7 kabla ya mwisho wa siku rasmi ya biashara huko New York kufika.
Hisa za Apple ziliathirika wiki iliyopita kufuatia ripoti za vizuizi kutoka Wachina kwenye iPhones katika ofisi za serikali na vyombo vinavyoungwa mkono na serikali.
Apple ilisajili mapato ya Dola bilioni 15.8 Kutoka China katika robo ya hivi karibuni, takriban asilimia 20 ya mapato ya jumla. Watendaji walionyesha kuongezeka kwa mauzo ya China katika kipindi hicho ambacho mauzo ya jumla yalipungua.
"Tunaamini licha ya kelele kubwa Apple imepata faida kubwa ya hisa katika Soko la simu la China," Ives alisema.