Ilikuwa vigumu kuingia Orodha ya Forbes 400 ya watu Matajiri zaidi Marekani mwaka huu, kwani kiwango cha chini cha thamani kinachohitajika kutinga orodha hiyo ikifikia rekodi ya dola bilioni 2.9
Licha ya Mchezaji huyo wa mpira wa kikapu kujipatia dola milioni 90 katika kipindi kile alichokuwa akicheza, amejizolea mapato zaidi nje ya uwanja kwani uwekezaji huo umemfanya awe miongoni mwa Wamarekani matajiri zaidi.
Kwa miongo kadhaa, Jordan amekuwa akipata pato kutoka kwa kila kiatu cha Jordan, shati au soksi zilizouzwa na kampuni ya Nike ambayo ilikuwa ya kutosha kumletea mapato ya dola milioni 260 katika mapato ya makadirio (kabla ya kodi) katika mwaka uliopita pekee.
Aidha, pato lakke kuu pia limetoka klabu ya Charlotte Hornets. Mnamo Agosti, Jordan aliuza hisa nyingi katika timu hiyo ya NBA kwa thamani ya dola bilioni 3, ikiwa ni mara 17 ya thamani yake wakati alipopata kuwa mmiliki mkuu mnamo 2010.
Nguli huyo wa mpira wa kikapu alipata mojawapo ya ufanisi mkubwa wa biashara yake ya kupitia uuzaji huo wa mwezi Agosti.
Mapato hayo ni takriban mara tatu dola milioni 90 alizopata katika enzi alipokuwa akicheza kwa miaka 16.