Turkish airlines

Shirika la ndege la Turkish Airlines leo limefikia hatua muhimu tangu kuanzishwa kake baada ya kufikisha idadi ya abiria bilioni moja waliotumia usafiri huo.

Shirika hilo lilimzawadia abiria wake Mustafa Balci ambaye ndiye aliyekuwa wa bilioni moja kutumia usafiri huo zawadi ya kusafiri bure maili milioni moja.

Abiria huyo alikuwa akisafiri kwa ndege kutoka Istanbul kuelekea mkoa wa kusini mashariki mwa Uturuki huko Adiyaman.

"Kuishi uzoefu huu itakuwa kumbukumbu isiyoweza kusahaulika kwangu," Balci alisema.

Ahmet Bolat, mwenyekiti wa bodi na kamati ya utendaji ya Turkish Airlines, alisema: "Chapa yetu, ambayo imefikisha abiria bilioni 1 katika miaka 90, inalenga kubeba abiria bilioni 2 mwaka 2031."

Maili ya bonasi inaweza tumiwa kwa safari za ndege, hoteli, magari ya kukodisha na sehemu nyingine za safari kupitia Turkish Airlines.

Kwa sasa shirika la ndege la Turkish Airlines lina ndege 413 na zinasafiri hadi maeneo 342 - 289 ya kimataifa na 53 ya ndani.

AA