Hatimaye sekta za usafiri na Utalii za Kenya na Tanzania zinatazamiwa kujizolea tuzo katika vitengo mbalimbali baada ya kuwasilishwa kwenye orodha ya watakaowania tuzo za kila mwaka za Usafiri ulimwenguni 'World Travel Awards' zitakazotolewa kwenye hafla tarehe 15 Oktoba 2023.
Shirika la ndege la Kenya Kenya Airways, hifadhi ya taifa ya Masai Mara, Kenya pamoja na mbuga ya taifa ya Serengeti, Tanzania ni baadhi ya waliotajwa kuwania tuzo hizo kati ya vitengo vitakavyoshindaniwa kwa mujibu wa tuzo hizo.
Hifadhi bora ya Taifa Afrika 2023
- Hifadhi ya wanyama ya Kalahari ya Kati, Botswana
- Mbuga ya kitaifa ya Etosha, Namibia
- Mbuga ya kitaifa ya Bonde la Kidepo, Uganda
- Mbuga ya kitaifa ya Kruger, Afrika Kusini
- Hifadhi ya taifa ya Masai Mara, Kenya
- Mbuga ya taifa ya Serengeti, Tanzania
Shirika bora la ndege Afrika 2023
- Shirika la Ndege la Ethiopia
- Kenya Airways
- Ndege ya Royal Air Maroc
- RwandAir
- Shirika La Ndege la Afrika Kusini
- Tunisair
- Egypt Air
Uwanja bora wa ndege Afrika 2023
- Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town, Afrika Kusini
- Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Casablanca Mohammed V, Morocco
- Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Kenya
- Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Tanzania
- Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali, Rwanda
- Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Shaka, Durban, Afrika Kusini
- Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O. R. Tambo, Afrika Kusini
Kivutio bora cha watalii barani Afrika 2023
- Barabara ya Anga ya Hartbeespoort, Afrika Kusini
- Ziwa Malawi
- Mlima Kilimanjaro, Tanzania
- Eneo la hifadhi la Ngorongoro, Tanzania
- Delta ya Okavango, Botswana
- Piramidi za Giza, Misri
- Kisiwa cha Robben, Afrika Kusini
- Table Mountain, Afrika Kusini
- V&A Waterfront, Afrika Kusini
Pwani inayoongoza Afrika 2023
- Bazaruto, Msumbiji
- Cape Maclear, Malawi
- Cape Town, Afrika Kusini
- Dakhla, Morocco
- Pwani ya Diani, Kenya
- Pwani ya Nungwi, Tanzania
- Ghuba ya Plettenberg, Afrika Kusini
- Sharm El Sheikh, Misri
- Zanzibar, Tanzania
Bodi bora ya Utalii Afrika 2023
- Shirika la Utalii la Botswana
- Mamlaka ya Utalii Ya Misri
- Bodi ya Utalii Ya Gambia
- Mamlaka ya Utalii Ya Ghana
- Bodi ya Utalii Kenya
- Ofisi ya Kitaifa Ya Utalii Ya Morocco
- Bodi ya Utalii Ya Namibia
- Shirika la Maendeleo Ya Utalii La Nigeria
- Bodi ya Maendeleo Ya Rwanda
- Utalii wa Afrika Kusini
- Bodi ya Utalii Tanzania
- Tume ya utalii Zanzibar
Tanzania ilinyakua tuzo ya hifadhi bora ya taifa Afrika mwaka 2019.
Washindi watajulikana kwenye Sherehe ya Gala kwa washindi wa Afrika na Bahari ya Hindi 2023 itafanyika Dubai, UAE, tarehe 15 Oktoba 2023
TRT Afrika