Picha: Wizara ya Uchukuzi Kenya

Waziri wa Uchukuzi na Usafiri wa Anga wa Somalia Fardowsa Igal Osman alisema kuwa hatua hiyo itaondoa vizuizi kwa ndege zenye nambari za leseni za Somalia ambazo hapo awali hazikuweza kuja Kenya, kwani sasa zitaweza kuruka hadi Kenya na nambari za leseni za Somalia zilizosajiliwa nchini humo.

Makubaliano hayo yamejikita katika misingi minne ikiwa ni pamoja na haki za Trafiki (msongamano), mzunguko na uwezo, hisa na Mkataba wa Ushirikiano wa Kiufundi (TCA). Serikali hizo mbili zitaanzisha ushirikiano kamili katika usafiri wa anga, ili kudhibiti ndege ambazo zina leseni ya kuruka kati ya nchi hizo.

Kwa upande wake, Waziri wa Kenya wa Barabara na Uchukuzi Kipchumba Murkomen alibainisha kuwa makubaliano hayo pia yatafungua milango sio tu kwa shirika la ndege la taifa la Kenya la KQ bali pia kwa mashirika mengine ya ndege. Mashirika ya ndege ya KQ hayatahitajika tena kuandikia wizara ya Usafiri wa Somalia ili kupata vibali muhimu vya usafiri wa anga.

TRT Afrika