Zizipho anasema kuishi na phocommelia kumeunda mtazamo wake wa ulimwengu, /Picha: Zizipho.

Na Pauline Odhiambo

Unafanya nini wakati mtu kwenye kioo haonekani kamwe kama picha iliyofafanuliwa ya uzuri wa kuhitajika?

Zizipho Soldat, mtayarishaji wa maudhui wa Afrika Kusini anayeishi na ulemavu wa kuzaliwa, hukabiliwa na suali hili kila siku.

Zizipho ana maradhi ya phocomelia, hali ambayo mtu huzaliwa akiwa na ulemavu wa viungo au kukosa viungo. Katika kesi yake, mkono wake wa kushoto haujaundwa kikamilifu, wakati mguu wake wa kushoto ni mfupi sana kuliko wa kulia.

Lakini hii haijamzuia Zizipho kuwa mwanamitindo na kuanza kazi yake kwenye mitandao ya kijamii, akifafanua upya viwango vya kikomo vya tasnia ya mitindo na urembo duniani.

Zizipho anashukuru kwamba mashirika matatu ya wanamitindo yamemsajili, lakini njia ya kujikubali imekuwa na machungu.

Akiwa msichana mdogo alikua na ulemavu, alijitahidi kuelewa ni kwa nini watu walimtazama kwa njia tofauti. Unyanyapaa uliofuata uliifanya kuwa mbaya zaidi.

''Kimwili, niliona kwamba sikufanana na wasichana wengine, ingawa hilo halikunisumbua hadi unyanyasaji ulipoanza," anaiambia TRT Afrika.

Alipokuwa akikua, Zizipho alipatwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya kuonewa. Picha: Zizipho

Alipokuwa katika darasa la 12, Zizipho alikuwa akitumia dawa za mfadhaiko na kuonana na mtaalamu mara kwa mara.

Alipata faraja kwa kuandika kuhusu hisia zake katika jarida, akiimarisha ujuzi wake wa mawasiliano katika mchakato huo. Lakini mawazo ya giza hayakumuacha.

“Nilijiua. Nilihisi nisingeweza kustahimili. Akilini mwangu, kila mara kulikuwa na wazo hili kwamba nikifika umri fulani, na bado ninahisi hivi, nitakatisha maisha yangu, "anasimulia.

Mwanzo mpya

Kutazama wanamitindo wa kimataifa kama Naomi Campbell akitembea kwenye njia panda kungemtia moyo Zizipho, na akaanza kuwaza kuhusu kuwa mwanamitindo.

"Katika darasa la 12, niliandika barua kwa gazeti, nikisema ninataka kuwa mwana mitindo. Rafiki zangu waliipata, na wakacheka. Wakauliza, 'Unatakaje kuwa mwanamitindo? Hebu jitazame !'

Matamshi hayo ya dhihaka yanaweza kuwa yalimfanya Zizipho kuwa na uchungu lakini hayakuzuia azimio lake la kuwathibitisha wababe hao kuwa wamekosea. “Nilimwuliza Mungu, ‘Unawezaje kuumba mtu mzuri sana mwenye akili na utu mkubwa hivi, lakini mwili ni tofauti?’”

Zizipho kisha akaanza kujipiga picha na kuzituma kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii. Kisha akatafuta wakala wa uanamitindo kwa ajili ya picha za kitaalamu, kisha akaishia kuchezwa shere na wakala.

“Nilikuwa na akiba kwa ajili yakulipia picha zangu. Nilimlipa randi 600, ambayo ni sawa na dola 90 za Marekani, lakini alikimbia na pesa zangu. Alikuwa mdanganyifu pia. Alisema lazima nimtumie picha zangu za uchi ikiwa ninataka kuwa mwanamitindo. Nikiwa na miaka 17, nilikuwa mwerevu. sikufanya hivyo."

Wakala wa wanamitindo wa Uingereza walimsaini Zizipho mnamo 2020.. Picha: Zizipho.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 28 sasa anasema kipindi hicho vunja moyo sana kuliko alivyokuwa, na kubagiliwa kwa imani potofu za kitamaduni kuhusu hali yake.

"Unapokua, unasikia maneno 'ni ishara mbaya au adhabu kwa dhambi za wazazi au mababu zako'. Hayo ndiyo mawazo niliyoshughulika nayo hadi nilipokuwa mtu mzima vya kutosha kufanya utafiti wangu mwenyewe juu ya phocomela."

Si pekee yake

Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu milioni 80 barani Afrika ni walemavu, ikiwa ni pamoja na wale walio na hali ya afya ya akili, kasoro za kuzaliwa, na matatizo mengine ya kimwili.

Zizipho anasema baadhi ya picha alizochapisha kwenye mitandao ya kijamii hazikupokelewa vyema kila mara. Ingawa kukataliwa kungemfanya ajisikie vibaya kwa muda, hamu ya kuwa mwanamitindo haikumwacha kamwe.

“Baadhi ya watu walisema nina maadili mabaya. Walishangaa ni nini mtoto wa miaka 16 alikuwa akifanya, akiwa amevaa sidiria. Lakini nia yangu ilikuwa kuwa kile nilichotaka kuwa, "anasema.

Kadiri ufuasi wa mitandao ya kijamii wa Zizipho ulivyokua kwa miaka mingi, ndivyo imani yake ilivyoongezeka. Hatimaye alipata ujasiri wa kukaribia wakala mwingine wa uanamitindo mnamo 2020.

“Nikawaambia huenda sina viungo vyote vinne, lakini naweza pozi, na walihitaji kunisaini, nikawaambia nimepata madoido na mapozi kusainiwa. Nawezaje kuwa mrembo kiasi hii na nikose kusainiwa? Walipenda kujiamini kwangu na kunitia saini. Shirika lingine lililo nchini Uingereza lilinisaini baada ya kuona picha zangu."

Nchini Uingereza, data iliyokusanywa na Maktaba ya House of Commons inaonyesha kuwa hadi watu milioni 14 wanaishi na ulemavu, lakini ni asilimia 0.02 tu ya kampeni za mitindo zinazoonyesha wanamitindo wenye ulemavu wa wazi.

Licha ya takwimu, Zizipho ana matumaini kwamba idadi ya wanamitindo wenye ulemavu itaongezeka huku wito wa kupanuliwa zaidi ulingo huo na uboreshaji wa mwili ukifungua nafasi za kusherehekea urembo katika aina zake zote tofauti.

Zizipho anasema tiba ilimsaidia kukabiliana na tatizo la afya ya akili. /Picha: Zizipho.

Raia huyo wa Afrika Kusini shupavu anaamini kwamba kuunganisha watu wenye ulemavu katika sekta tofauti ni muhimu katika kuzuia fikra za kujitoa uhai miongoni mwa watu wachache wenye ulemavu.

"Mwaka jana, nilipoteza rafiki ambaye alikuwa na ulemavu. Hakuweza kuvumilia kupitia changamoto za maisha kama mlemavu, na aliamua kukatisha maisha yake," anasema Zizipho. "Siku aliyofariki, alichapisha mtandao wa WhatsApp akisema alikuwa anaumwa.''

Kupoteza rafiki kulimlazimisha Zizipho kurudi katika hali ya mfadhaiko, na yeye pia alifikiria kujikatia uhai. Vipindi vya matibabu ambavyo amekuwa akihudhuria tangu utoto kwa bahati nzuri vilimsaidia kukabiliana na hasara hiyo.

"Kwangu mimi, msongo wa mawazo ni kama uraibu, na matibabu ndio rehab ninayohitaji ili kuishi. Tiba imeniweka hai,” anasema.

Zizipho pia amejifunza kustahimili kupewa "majukumu ya walemavu" katika kazi yake ya uanamitindo.

"Kuna majukumu machache sana kwa watu wanaofanana nami. Wakala wangu wa kwanza wa uanamitindo ungeniweka tu katika majukumu mahususi kwa watu wenye ulemavu," anaeleza.

"Nataka kujitokeza kwenye tamasha lolote na kusema, 'Ulisema unataka msichana mwenye umri wa miaka ishirini na mwenye nywele ndefu? Mimi ndiye unayetafuta. Nina mwili tofauti tu'."

Zizipho anatahadharisha juu ya miundo potofu yenye ulemavu. /Picha: Zizipho.

Anashukuru mitandao ya kijamii kuwa chombo madhubuti ambacho watu wenye ulemavu wanaweza kudhibiti jinsi wanavyoonekana. Zaidi ya mitandao ya kijamii, ameboresha ujuzi wake wa uandishi kupitia blogu mbalimbali, akitoa maudhui yanayohusiana kuhusu maisha ya watu wenye ulemavu.

"Siku zote huwa nahimiza watu wanaofanana na mimi angalau wawe na kitu kwenye karatasi ambacho kinaweza kukuzungumzia katika masuala ya ujuzi," anasema Zizipho, ambaye alisomea sayansi ya mahusiano ya umma na mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Walter Sisulu huko Mthatha nchini Afrika Kusini.

Pia ameongoza filamu kuhusu ulemavu. Zizipho anatamani siku moja kutembea kwenye jukwaa la mamodo Wiki ya Mitindo huko New York na Paris, pamoja na kuchapisha kitabu na kuanzisha chapa ya vipodozi vinavyofaa ulemavu.

"Nataka kuunda chapa ya urembo ambayo ni ya kila mtu, lakini pia inayoweza kubadilika. Chukua, kwa mfano, bomba la kawaida la lipstick, lakini fikiria juu ya mtu asiye na mikono ambaye anataka kupaka lipstick. Nataka kutengeneza bidhaa za urembo ambazo zinavutia sana watu wenye ulemavu wanaweza kutumia kwa urahisi."

TRT Afrika