Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia amepiga simu tofauti na viongozi hasimu wa Sudan, akizitaka pande hizo mbili kurudisha uhusiano.
Faisal bin Farhan alijadili "maendeleo ya hivi punde nchini Sudan" na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa jeshi la Sudan na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, kiongozi wa Kikosi cha dharura (RSF).
"Waziri wa Mambo ya Nje alisisitiza umuhimu wa kujitolea kwa pande zote za Sudan ili kulinda raia na usalama wa njia za kibinadamu kwa ajili ya kuwasili kwa misaada ya kimsingi," wizara ya mambo ya nje ya Saudi ilisema katika taarifa yake Jumanne. .
Farhan alianzisha upya wito wa Saudi Arabia wa utulivu, akitoa kipaumbele kwa maslahi ya taifa [ya Sudan], kusimamisha aina zote za ongezeko la uhasama wa kijeshi na kutafuta suluhu la kisiasa ambalo linahakikisha kurejea kwa utulivu.
Jaribio la kwanza katika muda mrefu
Simu hizo mbili zilikuwa za kwanza kwa muda mrefu zilizohusisha majenerali hao wawili moja kwa moja katika kujadili mzozo wa Sudan.
Saudi Arabia haikufichua kwa undani kile Al-Burhan na Dagalo walisema wakati wa mazungumzo yao ya simu na Farhan.
Nchi hiyo ya Mashariki ya Kati inawakaribisha wawakilishi wa pande hasimu kwa mazungumzo katika mji wa bandari wa Jeddah. Serikali ya Marekani inashiriki mazungumzo hayo.
Al-Burhan na Dagalo walitofautiana huku Sudan ikijiandaa kurejea katika utawala wa kiraia, na hivyo kusababisha vita vilivyozuka Aprili 15. Pande zote mbili zinadai kuwa viongozi halali wa Sudan.
Mzozo wa Sudan tangu wakati huo umeshindwa kudhibitiwa, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 2,000 na wengine zaidi ya milioni 2.2 kuhama makazi yao, kulingana na UN.
Kuna usitishaji vita unaoendelea nchini Sudan ulioanza Jumatatu na unatarajiwa kuendelea hadi Jumatano saa kumi na mbili asubuhi kwa saa za huko.
Mrengo unaoongozwa na Al-Burhan umeshutumu upande wa Dagalo kwa kukiuka makubaliano ya muda.