Kiongozi wa Mashtaka nchini Sudan umetuhumu Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdalla Hamdok kwa "kuchochea vita dhidi ya taifa" na mashtaka mengine ambayo yanaweza kubeba hukumu ya kifo, kulingana na televisheni ya taifa.
Ofisi ya mwendesha mashtaka ana heshimu Mkuu wa Majeshi Abdel Fattah al Burhan, ambaye vikosi vyake vya kijeshi vimekuwa vitani tangu Aprili 2023 na kiongozi wa kijeshi Mohamed Hamdan Dagalo.
Watu wengine 15, wakiwemo waandishi wa habari na wanasiasa ambao kama Hamdok wanaishi nje ya nchi, wanakabiliwa na mashtaka kama hayo "yenye kukiuka katiba."
Hamdok, mwanasiasa mashuhuri zaidi wa kiraia wa Sudan, alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa nchi hiyo katika kipindi kigumu cha mpito kufuatia maasi baada ya miongo kadhaa chini ya utawala wa Omar al Bashir.
Novemba 2021, nchi hiyo ilitia saini makubaliano ya kumrejesha madarakani Abdalla Hamdok kama Waziri Mkuu. Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alitia saini mkataba huo na Hamdok kurejesha mpito kwa utawala wa kiraia karibu mwezi mmoja baada ya mapinduzi ya kijeshi.
Hamdok aliwekwa kizuizini nyumbani kwake katika baada ya kutokea mapinduzi ya Oktoba 2021 yaliyofanywa na washirika wa zamani Dagalo na Burhan.
Baada ya kurejeshwa kwa muda mfupi, Hamdok alijiuzulu Januari 2022 na kukimbilia Abu Dhabi. Tangu wakati huo ameibuka tena kama sehemu ya muungano mpya unaojulikana kama Taqadum.
Vita vya Sudan vimegharimu maisha ya maelfu ya watu na kuwakosesha makazi zaidi ya watu milioni 8.5, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Hamdok amekuwa katika mazungumzo kwa miezi kadhaa na viongozi wa Sudan na wa kikanda katika jitihada za kumaliza vita.
Juhudi hizi zimemfanya Dagalo, ambaye anaongoza Kikosi cha Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF), kumuunga mkono Hamdok. Dagalo, mfanyabiashara wa zamani wa ngamia na kondoo, alipata umaarufu chini ya Bashir, ambaye aliwaachilia wanamgambo waliojulikana kama Janjaweed baada ya uasi wa makabila madogo kuanza huko Darfur mwaka 2003.
Operesheni ya wanamgambo hao ilisababisha mashtaka ya uhalifu wa kivita dhidi ya Bashir na wengine.
Wakati maafisa wa usalama walipowashambulia waandamanaji wanaounga mkono demokrasia mjini Khartoum mnamo Juni 2019 baada ya kupinduliwa kwa Bashir, ilikuwa ni RSF ambayo mashahidi walisema ilikuwa mstari wa mbele katika umwagaji damu, na kuua watu wasiopungua 128.
Hata hivyo, kuungwa mkono kwa Dagalo kwa mshirika wa kiraia Hamdok kunatoa fursa ya kupata uhalali wa kimataifa, wachambuzi wamesema.
Tom Perriello, mbunge wa zamani aliyeteuliwa hivi karibuni katika nafasi mpya ya mjumbe maalum wa Marekani kwa Sudan, alisema kuwa mazungumzo ya kumaliza vita vya Sudan yanaweza kuanza karibu Aprili 18.