Watu 8 wafariki dunia baada ya helikopta kudondoka baharini nchini Nigeria

Watu 8 wafariki dunia baada ya helikopta kudondoka baharini nchini Nigeria

Watu wanane wanahofiwa kufa baada ya helikopta hiyo kudondoka katika bahari ya Atlantiki.
Ajali hiyo ilihusisha helikopta aina ya Sikorsky 5K76 yenye usajili namba 5NBQG, ambayo ilikuwa ikielekea katika kisima cha kuchimba mafuta kusini mwa Nigeria, siku ya Oktoba 24, 2024./Picha: AA  

Helikopta ya Kinigeria ambayo ilikuwa na abiria wanane, imedondoka ndani ya bahari ya Atlantiki, Wizara ya anga ya nchi hiyo imethibitisha.

Tukio hilo lilitokea majira ya asubuhi ya Oktoba 24, 2024 karibu na mji wa Bonny Finima ulio kusinimashariki mwa jimbo la Rivers.

Ajali hiyo ilihusisha helikopta aina ya Sikorsky 5K76 yenye usajili namba 5NBQG, ambayo ilikuwa ikielekea katika kisima cha kuchimba mafuta kusini mwa Nigeria.

Helikopta hiyo ilikuwa chini ya umiliki wa kampuni ya East Wind Aviation.

"Mamlaka za usalama zimejulishwa kuhusu tukio hilo, huku vikosi vya uokoaji vikienda eneo la tukio," alisema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Anga ya Nigeria, Odutayo Oluseyi, katika taarifa yake iliyotolewa siku ya Alhamisi.

Milli mitatu ilikuwa imeopolewa katika eneo la tukio, kulingana na Wizara hiyo.

TRT Afrika