Watu 4 wauawa katika shambulizi ya msafara wa wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani nchini Nigeria

Watu 4 wauawa katika shambulizi ya msafara wa wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani nchini Nigeria

Watu wenye silaha walikuwa wamevizia magari yaliyokuwa yamewabeba maafisa wa ubalozi wa Marekani katika jimbo la Anambra
Msemaji wa polisi Tochukwy Ikenga alisema watu wenye silaha walivizia msafara huo katika eneo la mtaa wa Ogbaru kusini mashariki mwa jimbo la Anambra | Picha: AA

Takriban watu wanne waliuawa Jumanne wakati watu wenye silaha walipofyatua risasi kwenye msafara uliokuwa na wafanyakazi wa ubalozi mdogo wa Marekani, polisi walisema.

Msemaji wa polisi Tochukwy Ikenga alisema watu wenye silaha walivizia msafara huo katika eneo la mtaa wa Ogbaru kusini mashariki mwa jimbo la Anambra.

"Wapiganaji hao waliwaua askari wawili wa Jeshi la Polisi na wafanyakazi wawili wa Ubalozi mdogo na kuteketeza miili yao pamoja na magari yao," alisema.

Alisema washambuliaji hao pia waliwateka nyara maofisa wawili wa polisi na dereva wa gari la pili na kukimbia.

"Hakuna raia wa Marekani aliyekuwa kwenye msafara huo," alisema Ikenga, akithibitisha taarifa iliyotolewa mapema na Ikulu ya Marekani.

Kikosi cha operesheni ya kukabiliana na uhalifu tayari kinawafuata watu wenye silaha ili kuwaokoa waliotekwa, alisema.

Wakazi wa eneo hilo walisema kuwa wafanyakazi hao walikuwa kwenye misheni ya kibinadamu katika eneo hilo.

AA