Na Charles Mgbolu
Aina ya muziki ya 'Afrobeats' inazidi kujulikana duniani kote huku nyota wake wakishinda tuzo za grammy, wakifurahia ushabiki mkubwa wa nje ya nchi na kufanya ziara tofauti duniani.
Wanamuziki wa Nigeria wamefanya lebo mingi za muziki zinazoongoza duniani na wameshirikiana na nyota tofauti wa kimataifa.
Lakini mafanikio yao ya kimataifa kwa sasa ni chanzo cha mabishano nyumbani, ambapo waandaaji wa hafla na mashabiki wanawashutumu kwa madai ya usaliti kwa kusisitiza kulipwa kwa dola za Kimarekani kwa maonyesho ya ndani.
Kiini cha mzozo huo ni cha pande mbili: Kwanza, uchumi wa Nigeria unapitia nyakati ngumu.
Pili, mashabiki wengi wanahisi maonyesho ya ndani yanapaswa kuwa fursa kwa wanamuziki kurudisha shukrani kwa mashabiki wao wa nyumbani ambao waliwajenga.
Mafanikio ya kifedha
Wazo hapa ni kuwa wasanii hao tayari wamepata mafanikio ya kifedha kwa kufanya hafla za kimataifa.
DJ wa eneo hilo Oladotun Ojuolape Kayode, almaarufu Do2dtun, alizua mzozo huo kwa kusema kuwa kusisitiza malipo kwa dola za Marekani ni kuwatenga wanamuziki hao kutoka kwa mashabiki wao wa nyumbani.
‘’Sasa unawatoza watu wako kwa dola, basi sahau mshikamano kati yako na watu wako. Ni jambo la ajabu kabisa,’’ aliandika kwenye X, hapo awali Twitter.
Shabiki, mmoja anayejiita @gbana_producer, kwa mtandao aliwakumbusha wasanii nyakati ambazo walitegemea sana Wanigeria kabla hawajakua wakubwa katika uwanja wa muziki duniani.
’Wasanii wa Afrobeats siku hizi ambao wana mashabiki wa Nigeria na kufikia hatua ya kimataifa kupata malipo zaidi kutoka kwa nchi za kigeni wanaanza kuongea vibaya kwa Wanigeria ambao waliwapa umaarufu awali,’’ aliandika kwenye X.
" Hata hawafanyi maonyesho hapa tena,’’ aliandika Kaybest mwingine kwenye X.
Dotun alikuwa na jibu kwa hili.
‘’Ilianza miaka miwili iliyopita. Sasa ni mbaya zaidi. Mashirika yamefuta mipango ya kuhusisha wasanii hao ya mwisho wa mwaka; watangazaji wa show hawawezi kulipa. ‘
" Tutaimba nyimbo zako kwa niaba yako," aliandika.
Mtangazaji huyo maarufu wa redio, hata hivyo, alitajwa katika mijadala hiyo, huku baadhi wakisisitiza kuwa tasnia nzima ina hatia na kwamba hata watangazaji wa redio na ma-DJ pia huwatoza wasanii wanaokuja kwa dola kabla ya nyimbo zao kuchezwa kwenye redio.
Dotun, hata hivyo, alikanusha madai hayo lakini alikubali kwamba tatizo la kutoza dola limeenea kwa wasiwasi katika tasnia ya burudani ya Nigeria.