Rwanda imeanzisha mfumo mpya wa malipo ya ada ya usafiri wa umma.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma nchini Rwanda (RURA) imezindua mfumo wa abiria kulipia gharama za huduma za usafiri wa mabasi ya umma kulingana na umbali wa eneo moja hadi jingine ndani ya jiji la Kigali.
Mfumo huo utakuwa mbadala wa ule wa awali ambao serikali ilikuwa inapanga bei bila kuzingatia umbali wa sehemu anayokwenda msafiri husika.
Kupitia utaratibu huo, msafiri huchagua njia anayokwenda kwa kuchanja kadi kadi yake kwenye mita maalumu, huku mita hiyo ikitoza kiwango cha nauli kulingana na umbali anaokwenda msafiri huyo.
Kulingana na mfumo huo, gharama za umbali wa kilomita moja ni nusu ya Dola Moja ya Kimarekani.
Liwapo safarini, basi hilo huanza kukutoa nauli halisi kulingana na kilomita na msafiri hurudishiwa chenji yake kwa njia ya kuchanja pale anaposhuka.
Takribani sekunde 10 hadi 15 hutumika katika kuchakata na kumrudhishia chenji abiria, kupitia mfumo huo mpya.
Kulingana na Beata Mukangabo, ambaye anasimamia kanuni za usafiri ndani ya RURA, mfumo huo mpya unatarajiwa kuleta mageuzi katika huduma za usafiri wa umma nchini Rwanda.
“Kupitia mfumo huu, abiria hawatolazimika tena kulipia njia nzima,” alieleza Mukangabo.