Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MINUSMA ulitumwa Mali mwaka 2013. / Picha: AFP

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali wametangaza kuondoka katika kambi mbili katika eneo la Kidal.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuleta utulivu unaojulikana kama MINUSMA ulipangwa kuondoka kwenye kambi hizo katikati ya Oktoba.

Jeshi la Mali, likitarajia kuondolewa kwa Umoja wa Mataifa, lilitua ndege mbili katika kambi moja ya Tessalit, maafisa wawili wa uwanja wa ndege walisema.

Ndege hizo zilileta wanajeshi wa serikali pamoja na mamluki wa Urusi kutoka kundi la Wagner, maafisa hao walisema.

Kambi ya Tessalit iko karibu na uwanja wa ndege na ilikuwa na wafanyikazi wengi wa Chad chini ya bendera ya UN.

Ndege ilishambuliwa

Jeshi la Mali lilichapisha kwenye mitandao ya kijamii kwamba ndege moja ilishambuliwa lakini ikafanikiwa kutua na kuondoka bila matatizo baada ya ngome za adui "kukatwa makali " na jeshi la wanahewa.

"Katika hali ya taharuki , ujumbe huo uimeanza mchakato wa kujiondoa katika kambi zake katika eneo la Kidal, kuanzia Tessalit na Aguelhok," MINUSMA ilisema katika taarifa yake.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa walitaja ufyatuaji risasi wakati wa asubuhi kama unaonyesha "kuzorota kwa kasi kwa hali ya usalama kwa maisha ya mamia ya askari kwa ajili ya amani."

Uondoaji ungekamilika "haraka iwezekanavyo, pamoja na uwezekano wa kuharakisha kujiondoa" kutoka kambi ya tatu, katika mji wa Kidal yenyewe, ambayo ilikuwa imepangwa katikati ya Novemba.

Kikosi tawala cha Mali, ambacho kilichukua mamlaka mnamo 2020, kiliitisha mwezi Juni misheni hiyo - ambayo ilikuwa imetumwa tangu 2013 - iondoke nchini licha ya kuwa ilidhibiti uasi wa wanamgambo na mgogoro mkubwa wa pande nyingi.

TRT Afrika