Rais Paul Kagame, ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala cha Rwanda Patriotic Front  anagombea tena kiti cha urais/ Picha  ya NEC.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Rwanda (NEC), imatangaza kuwa hadi sasa ni wagombea watatu tu ndio wanaokidhi matakwa ya kisheria kugomeba urais hadi sasa.

Mwenyekiti wa tume hii Oda Gasinzigwa alisema Tume ilipokea wagombea tisa wa urais na baada ya kuwachuja, watatu walitimiza vigezo.

Rais Paul Kagame, ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala cha Rwanda Patriotic Front (RPF Inkotanyi), Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Green Party of Rwanda, Frank Habineza na mgombea wa kujitegemea Philippe Mpayimana ndio waliotimiza vigezo.

Wagombea ambao wanakiuka matakwa hayo ni Herman Manirareba, Innocent Hakizimana, Fred Sekikubo Barafinda, Thomas Habimana, Diane Rwigara, na Jean Mbanda.

Kwa mujibu wa sheria, wagombea ambao faili zao hazijakamilika wanaweza kuwasilisha nyaraka zao ambazo hazijakamilika kabla ya Juni 14, tarehe ambayo orodha ya mwisho itawekwa wazi, kwa mujibu wa NEC.

Paul Kagame

Rais wa sasa wa Rwanda, Paul Kagame, ambae anapeperusha bendera ya Rwanda Patriotic Front (RPF-Inkotanyi) - chama tawala nchini humo - aliwasilisha ombi lake Ijumaa, Mei 17.

Kagame amekuwa rais wa Rwanda tangu mwaka 2000.

Mnamo 2017, alichaguliwa tena kuwa rais baada ya ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 98 ya jumla ya kura zilizopigwa.

Philippe Mpayimana

Mgombea huru wa urais Philippe Mpayimana, alisisitiza haja ya maendeleo endelevu kwa Rwanda na watu wake.

Ni jaribio la Philippe Mpayimana la pili kwa nafasi ya urasi baada ya kugombea tena mwaka 2017/ Picha: Wengine 

Hilo ni jaribio lake la pili kwa nafasi ya urasi baada ya kugombea tena mwaka 2017 alipopata asilimia 0.72 ya kura zote katika uchaguzi ambao Kagame alishinda.

Mpayimana sasa ni mtaalamu mkuu anayesimamia ushirikishwaji wa jamii katika Wizara ya Umoja wa Kitaifa na Ushirikiano wa Kiraia (MINUBUMWE), nafasi ambayo ameishikilia tangu Novemba 2021.

NEC itatangaza orodha ya muda ya wagombea kwenye tovuti yake Juni 6, na orodha ya mwisho Juni 14.

Frank Habineza

Frank Habineza, mwenyekiti wa chama cha Democratic Green Party of Rwanda, anajaribu kuwa mkuu wa nchi tena, baada ya kushindwa katika uchaguzi wa urais wa 2017 ambapo alipata asilimia 0.45 ya kura zote.

 Frank Habineza ni mwenyekiti wa chama cha Democratic Green Party of Rwanda/ Picha : Frank Habineza

Ajenda yake imekuwa ni kutetea mahitaji ya chakula na usalama kwa kila mwananchi wa Rwanda.

TRT Afrika