Jumla ya wachimba migodi 87 walitoka katika mgodi huo siku ya Alhamisi . / Picha: Reuters

Mamlaka nchini Ghana imewakamata makumi ya wachimbaji haramu wa dhahabu ambao walitumia siku kadhaa chini ya ardhi baada ya kuvamia mgodi wa dhahabu katika mji wa kusini wa Obuasi, vyombo vya habari vya ndani vinaripoti.

Jumla ya wachimba migodi 87 walitoka katika mgodi huo siku ya Alhamisi baada ya kupitia sehemu zisizo idhinishwa za kuingia. Inasemekana walikataa kuondoka mgodini kwa kuhofia kukamatwa baada ya viingilio kufungwa.

Awali katika kampuni kubwa ya uchimbaji madini ya Anglogold Ashanti, inayomiliki mgodi huo, ilisema njia kuu ya kutokea bado iko wazi na baadhi ya wachimbaji hao wametoka kwa miguu, kwa mujibu wa taarifa.

"Hakuna mtu chini ya ardhi ambaye amezuiliwa kwa njia yoyote ile na njia kuu ya kutokea mgodini inabaki wazi," ilisema.

Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Obuasi Mashariki Faustina Amissah alisema wachimbaji hao walikuwa sehemu ya kundi kubwa lililovamia mgodi huo siku ya Jumatatu. Wale waliokamatwa walikuwa wameachiliwa kwa dhamana, alisema

Wakazi wa eneo hilo walivamia na kuharibu mali siku ya Jumanne kupinga kukamatwa kwa baadhi ya wachimba migodi ambao walikuwa wameondoka kwa hiari.

"Mji umetulia, kila mtu anaendelea na maisha yake ya kawaida. Kila kitu kimedhibitiwa," Bi Amissah aliwaambia waandishi wa habari.

TRT Afrika