Waandishi Wasio na Mipaka(RSF) walaani uamuzi wa Israeli kukifunga kituo cha Al Jazeera

Waandishi Wasio na Mipaka(RSF) walaani uamuzi wa Israeli kukifunga kituo cha Al Jazeera

Serikali ya imepiga kura ya kufunga ofisi za Al Jazeera nchini humo.
 Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema Jumapili kwamba serikali yake imepiga kura kwa kauli moja kufunga ofisi za eneo la shirika la utangazaji linalomilikiwa na Qatar Al Jazeera./Picha: Getty

"Bila kutoa sababu za msingi, serikali ya Israeli imepitisha uamuzi wa kusitisha matangazo ya Al Jazeera", ilisema taasisi hiyo ya RSF kupitia ukurasa wake wa X.

RSF ililaani vikali "sheria kandamizi" dhidi ya kituo hicho kinachomilikiwa na Qatar, kwa madai kwamba kinatangaza hujuma ya Israeli katika Ukanda wa Gaza, ambayo imeua zaidi ya Wapalestina 34,600 tangu Oktoba 7, 2023.

Katika taarifa yake ya Jumapili, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aliweka wazi nia yake nchi kukifunga kituo hicho.

Kituo cha Al Jazeera kina ofisi na wawakilishi nchini Israeli.

AA
TRT Afrika