Rais wa zamani wa Ivory Coast Gbagbo alishtakiwa na ICC kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu lakini akaachiliwa huru mwaka wa 2021. Picha: AFP

Hati ya kwanza ya kukamatwa kwa aliyekuwa Rais wa Sudan Omar Hassan Ahmad Al Bashir ilitolewa tarehe 4 Machi 2009 na ya pili tarehe 12 Julai 2010.

Mshukiwa bado yuko huru kwani hakuna nchi ambayo ilimkamata na kumpeleka ICC.

Bashir anashtakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki huko Darfur, Sudan tangu 2009.

Omar al-Bashir aliongoza Sudan kuanzia 1989 hadi 2019 kabla ya kuondolewa madarakani na jeshi/ Picha: Wengine 

ICC inasema kuwa hadi Omar Al Bashir atakapokamatwa na kuhamishiwa kwenye makao makuu ya mahakama hiyo iliyo The Hague, kesi hiyo itasalia katika hatua ya Utangulizi.

ICC inasema haiwezi kuwahukumu watu binafsi kama hawapo hawapo mahakamani.

Tarehe 11 Aprili 2019, Bashir aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi. Septemba 2019 uongozi wa Sudan ulichukuliwa na Baraza la Kijeshi la Mpito.

Baraza hilo hata hivyo lilikataa kumpeleka Bashir katika mahakama ya ICC na likasema litamfungulia mashtaka ndani ya nchi.

Joseph Kony anayedaiwa kuwa kamanda mkuu wa kikundi cha waasi cha Uganda cha Lord's Resistance Army hajawahi kukamatwa/ Picha Wengine 

Hati ya kukamatwa kwa Joseph Kony anayedaiwa kuwa kamanda mkuu wa kikundi cha waasi Uganda, cha Lord's Resistance Army (LRA) ilitolewa Julai 8, 2005.

Anashtakiwa kwa makosa 36 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, unaodaiwa kufanywa kati ya 1 Julai 2002 hadi 31 Disemba 2005 kaskazini mwa Uganda.

Hajawahi kukamatwa.

Saif al-Islam Qaddafi mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi / Picha: Getty 

Hati ya kukamatwa kwa Seif Al-Islam Gaddafi ilitolewa tarehe 27 Juni 2011.

Hayuko chini ya ulinzi wa Mahakama kwani hakuna nchi iliyomkata kwa niaba ya mahakama.

Mahakama ilifunga kesi zao baada ya kufariki

Kesi hiyo pia ilihusisha mashtaka ya Muammar Gaddafi na Abdullah Al-Senussi katika hati iliyotolewa tarehe 27 Juni 2011.

Kesi dhidi ya Abdullah Al-Senussi ilitangazwa kutokubalika tarehe 11 Oktoba 2013.

Mahakama ya ICC ilitoa hati ya kukamtwa kwa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi  27 Juni 2011:  Picha: Getty 

Kesi dhidi ya Muammar Gaddafi ilikatishwa tarehe 22 Novemba 2011, kufuatia kifo chake.

Hati ya kukamatwa ilitolewa kwa muhuri dhidi ya Paul Gicheru na Philip Kipkoech Bett mnamo 10 Machi 2015 na kutolewa tarehe 10 Septemba 2015 kwa makosa dhidi ya usimamizi wa haki yanayojumuisha kushawishi mashahidi kwa ufisadi katika kesi ya Kenya.

Mnamo tarehe 14 Oktoba 2022, Mahakama hiyo ilisitisha kesi dhidi ya Paul Gicheru kufuatia uthibitisho wa kifo chake.

Mnamo tarehe 2 Novemba 2020, Paul Gicheru alijisalimisha katika mamlaka ya Uholanzi kwa mujibu wa hati ya kukamatwa kwa makosa dhidi ya usimamizi wa haki yanayojumuisha kuwashawishi mashahidi wa Mahakama kwa ufisadi.

Mahakama ilitupilia mbali kesi

Mnamo tarehe 14 Oktoba 2022, Mahakama hiyo ilisitisha kesi dhidi ya Paul Gicheru kufuatia uthibitisho wa kifo chake.

Uhuru Kenyatta na William Ruto wote wakiwa mawaziri wakati huo, walishitakiwa katika mahakama ya ICC / Picha: Reuters  

Akiwa naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha wa Kenya, Uhuru Kenyatta alipata wito wa kuwasilishwa 8 Machi 2011.

Mashtaka yake yalikuwa ya uhalifu dhidi ya binadamu yanayodaiwa kutendwa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007-2008 nchini Kenya.

Mwendesha mashtaka aliondoa mashtaka hayo Disemba 2014.

Nae akiwa waziri wa zamani wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia wa Kenya wakati huo na Mbunge wa Eldoret Kaskazini wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi, William Ruto alipata wito wa mahakama ya ICC 8 Machi 2011.

Alishtakiwa kwa uhalifu dhidi binadamu ikiwemo mauaji, uhamisho wa watu kwa nguvu, na mateso, yanayodaiwa kufanywa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007-2008 nchini Kenya.

Kesi dhidi ya William Samoei Ruto na mwengine Joshua Arap Sang ilikatishwa mnamo 5 Aprili 2016.

Kesi ambazo mahakama ya ICC huangalia

Mahakama hii inaelezea katika tovuti yake kuwa ina uwezo wa kufanya kesi aina nne. Kwanza, jinai ya mauaji ya halaiki. Hii inaangaliwa ikiwa washtakiwa wana dhamira mahususi ya kuharibu kwa jumla au kwa sehemu kikundi cha kitaifa, kikabila, rangi au kidini kwa kuua washiriki wake au kwa njia nyengine.

ICC pia inahusika katika kesi za uhalifu wa kivita ambazo ni ukiukaji mkubwa wa mikataba ya Geneva katika mazingira ya vita  Picha: AFP

Pili, ICC inaweza kushtaki uhalifu dhidi ya ubinadamu, ambao ni ukiukwaji mkubwa unaofanywa kama sehemu ya shambulio kubwa dhidi ya raia yeyote. Aina 15 za uhalifu dhidi ya ubinadamu zilizoorodheshwa katika Mkataba wa Roma ni pamoja na makosa kama vile mauaji, ubakaji, kifungo, upotevu wa nguvu, utumwa - hasa wa wanawake na watoto, utumwa wa ngono, mateso, ubaguzi wa rangi na uhamisho.

ICC pia inahusika katika kesi za uhalifu wa kivita ambao ni ukiukaji mkubwa wa mikataba ya Geneva katika mazingira ya vita na ni pamoja na, kwa mfano, matumizi ya askari watoto, mauaji au mateso ya watu kama vile raia au wafungwa wa vita, kuelekeza mashambulizi kwa makusudi dhidi ya hospitali, makaburi ya kihistoria, au nyumba za ibada, elimu, sanaa, sayansi au madhumuni ya hisani.

ICC pia inaweza kufanya kesi inayohusisha uhalifu wa uchokozi. Hii inahusisha matumizi ya nguvu ya kijeshi na Serikali dhidi ya mamlaka, uadilifu au uhuru wa nchi nyingine.

TRT Afrika