Vikosi vya usalama vya Uturuki vimewashikilia watu 14 wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Daesh katika wigo wa Operesheni Bozdogan-22, Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Yerlikaya amesema katika taarifa yake.
Operesheni za wakati mmoja zilifanyika katikati mwa Eskisehir, kusini mashariki mwa Gaziantep, kaskazini mwa Samsun na mikoa ya kaskazini-magharibi ya Yalova na kurugenzi za polisi zinazohusika, chini ya uratibu wa ofisi za mwendesha mashtaka mkuu wa umma, Kurugenzi Kuu ya Usalama na Idara ya Kupambana na Ugaidi, alisema waziri huyo siku ya Jumanne.
Yerlikaya amesema watuhumiwa watani walikamatwa katika eneo la Eskisehir, sita Yalova, wawili Gaziantep na mwingine Samsun katika operesheni hiyo.
Wakiendesha zaidi ya operesheni elfu moja dhidi ya Daesh tangu Juni 1, 2023, polisi wa Uturuki waliwakamata zaidi ya washukiwa elfu mbili.
Uturuki, ambayo ni kati ya nchi za kwanza kuliita Daesh kama kundi la kigaidi, imekabiliwa na mashambulizi mengi kutoka kundi hilo.
Zaidi ya watu 300 wamepoteza maisha, na mamia zaidi wamejeruhiwa katika milipuko 10 ya kujitoa mhanga, mashambulio saba ya mabomu, na mashambulio manne ya kutumia silaha.