Uturuki imesikitishwa na ajali mbaya ya mgodini iliyotokea hivi karibuni huko Iran.
"Tumesikitishwa na vifo vilivyotokea na majeruhi kufuatia tukio lililotokea katika mgodi kwenye mji wa Tabas katika mkoa wa Khorasan Kusini wa Iran," Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilisema katika taarifa yake Jumapili.
Ankara inatoa salamu za rambirambi kwa watu wa Iran na kuwatakia ahueni ya haraka waliojeruhiwa.
"Ni imani yetu kuwa wale waliokwama mgodini wataokolewa haraka iwezekanavyo."
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian ameagiza uchunguzi ufanyike kujua chanzo cha tukio hilo.
Uchunguzi unaendelea
Takriban wafanyakazi 51 walipoteza maisha kufuatia mlipuko wa mgodi wa makaa ya mawe kaskazini mashariki mwa Iran, kulingana na vyombo vya habari vya nchi hiyo.
TRT Afrika