"Tangu mwaka 2020, migogoro inayotuzunguka na ya duniani imeonyesha wazi mtizamo muhimu wa ulimwengu kwa Uturuki," Altun amesema. /Picha: AA  

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun amesema kwamba Uturuki "inaendelea na safari yake kama mshirika, muhusika mkuu wa uchumi, na kivutio kikubwa" na ina jukumu muhimu kama "mshirika wa dunia" katika kutatua migogoro.

Akizungumza katika Bodi ya Uratibu wa Diplomasia ya Umma Alhamisi chini ya uenyekiti wake iliyofanyika Ikulu, Altun amesema kwamba rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefanya jitihada muhimu katika diplomasia ya umma na mawasiliano ya kimkakati kama moja wapo ya sehemu muhimu ya mikakati wa nchi, ikiwezesha kufikiwa kwa uanzishwaji wa mambo muhimu.

Amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa Bodi hiyo ya Uratibu, akisema kwamba, imeanzishwa kama taasisi jumuishi kurasimisha shughuli za diplomasia ya wazi na kuwezesha ufanisi wake kwa viwango vyote vya kitaifa.

Amesema, lengo la diplomasia ya umma ni "kuipa nguvu nembo ya Uturuki," na jitihada zinafanywa kutoa taarifa sahihi, kufanya mawasiliano ya kimkakati na uwezo wa teknolojia wa Uturuki.

Altun amegusia umuhimu wa kuwasilisha mtizamo wa Uturuki katika mambo ya kikanda na kimataifa katika hali ya uwazi, hasa yale yanayohusiana na maslahi ya Uturuki, yanayochangia amani na utulivu wa dunia.

Jukumu la Uturuki katika kutatua migogoro

Mwisho wa mkutano, Altun amesema kwamba kwa kufanya kazi katika uratibu wa diplomasia ya umma, ndio njia ya kuzalisha kazi iliyo bora.

Amesema, Uturuki ina uwezo mkubwa katika nyanja ya kimataifa na diplomasia ya umma, akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa jitihada zaidi na ushirikishaji ili kuboresha uwezo wake zaidi.

Akigusia kwamba, Uturuki iko katika eneo lililojaa migogoro na fursa, Altun amesema, "Tangu mwaka 2020, migogoro inayotuzunguka na ya duniani imeonyesha wazi mtizamo muhimu wa ulimwengu kwa Uturuki."

"Licha ya changamoto zote na majaribio, Uturuki inaendelea kusogea mbele na hatua sahihi katika uchumi wake. Katika hatua hii, Uturuki inaendelea na safari yake kama mshirika, muhusika mkuu wa uchumi, na kivutio kikubwa," amesema.

"Kwa upande mwengine, na utatuzi wa migogoro unaowezeshwa chini ya uongozi wa kidiplomasia wa Rais wetu, Uturuki kama muhusika wa dunia, inaonyesha uwepo wake kupitia majadiliano yenye tija," ameongeza.

TRT World