Fahrettin Altun, mkuu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, ameitaka dunia kuchukua hatua dhidi ya Israel, akiituhumu Tel Avivi kufanya mauaji ya halaiki dhidi ya Palestina.
"Serikali ya Israel ina kiu cha damu na machozi ya watu wasio na hatia. Kuna utawala wa mauaji Tel Aviv ambao umekuwa ukifanya mauaji ya halaiki mbele ya macho ya 'dunia iliyostaarabika,'" amesema Altun katika taarifa ambayo iliyowekwa katika mtandao wa X Jumatatu.
Altun ameyaelezea mashambulio ya Israel dhidi ya "walionyiwa chakula, wasio na makazi, na watu wasioweza kujihami" kama uchokozi wa moja kwa moja kwa binadamu.
"Kutojali uhai wa binadamu inadhalilisha hata serikali ya Israel. Inatia aibu, mbaya sana, na inachafua roho," ameongeza.
Uungaji mkono wa Marekani
Amesema kwamba muondelezo wa mashambilizi ya Israel yasingewezekana "bila usaidizi na uungwaji mkono wa mataifa makubwa wa ulimwengu He argued that Israel's continued occupation and dispossession of Palestinians would not have been possible "without the help and support of the global superpower of the world who has pretended to be brokering peace for so many years."
Alisema kuwa kuendelea kwa Israeli kuwachukua na kuwanyang’anya Wapalestina haingewezekana ”bila uungwaji wa nguvu kubwa ya ulimwengu ambao kwa miaka mingi imejifanya inaleta amani.”
“Israeli inatuambia sote waziwazi kwamba yote yalikuwa uwongo na udanganyifu. Lengo lao pekee lilikuwa kuendeleza na kupanua operesheni”, Altun alisema.
“Serikali ya Israel inadhani ina uhuru kamili wa kutenda kutokana na uungwaji wa Marekani. Lakini wao ni taifa lisilo na uhalali machoni mwa ulimwengu wote. Bila uhalali, hakuna serikali. Israeli itaingia katika historia kama serikali ambayo ilifanya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu,” alisema.