Muonekano wa sehemu ya Gaza iliyoharibiwa ikionekana kutoka uzio wa upande wa Israel, Mei 29, 2024. / Picha: Reuters

Rais wa China Xi Jinping ameitisha mkutano wa amani kuhusu mgogoro wa Israel katika Gaza iliyozingirwa, pindi alipokuwa akihutubia viongozi wa Kiarabu na wanadiplomasia katika mkutano uliofanyika Beijing.

China ni mwenyeji wiki hii wa Rais wa Misri Abdel Fattah el Sisi na viongozi wengine kadhaa wa Kiarabu ambao wanahudhuria mkutano unaotarajiwa kujadili mashambilizi yanayoendelea Gaza.

Akihutubia wajumbe, Xi amesema China inaunga mkono mkutano wa amani kutatua migogoro.

"Eneo la Mashariki ya Kati limebarikiwa na mustakbali wa maendeleo, lakini vita bado vinarindima," Xi amesema.

"Vita havipaswi kuendelea bila ukomo. Haki haitakiwa kukosekan milele," ameongeza .

TRT World