Altun amesisitiza jitihada za Israeli za kueneza propaganda yenye giza kupitia maafisa, wasomi, na vyombo vya habari. Amehakikisha, "Mara hii, hawatafanikiwa." / Picha: AA

Israeli inatengeza propaganda yake ya giza kutokana na uongo na inajaribu kueneza kupitia maafisa, wasomi, na vyombo vya habari, amesema Mkurugenzi wa Mawasiliano Fahrettin Altun.

"Katu hatutakata tamaa kwa kufichua upotoshaji wa Israeli na kudhihirisha ukweli katika ajenda ya dunia," amesema mkurugenzi.

Katika hotuba yake kwenye sherehe ya tuzo za TRT World Citizen Ijumaa, Altun amesema watu wenye fikra za kikoloni wanawatesa wale wenye fikra tofauti na wao. Amesisita, "Maonevu ya sasa ya Israeli dhidi ya Palestina, ni kiashiria cha fikra za kikoloni, ambayo inadhihirisha wazi matendo hayo."

Altun amesema mfumo wa sasa wa kimataifa, ambao umeanguka katika uso wa udhalilishaji wa Gaza, unaonyesha ni kwa nini kuna lazima ya kufanyika mabadiliko, na kusema, "Mashirika mengi ya utangazaji ya nchi za magharibi yanaonyesha kuunga mkono Israeli, kugemea upande mmoja, na kubadilisha ukweli."

"Katika mashambulizi ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya siku 100, Israeli inafanya propaganda za giza na upotoshaji kupitia vyombo vya habari vya kimataifa na makampuni ya mitandao ya kijamii."

Kutokana na uwajibikaji wa kibinadamu, Uturuki katu haibadiliki katika mashambulizi hayo, inasimama pamoja na watu wa Palestina wanaodhulumiwa, na itaendelea kufanya hivyo, amesema.

Altun amedokeza kwamba, mradi wa tuzo za Citizen Awards kupitia TRT ni jitihada za kila mmoja kuonyesha uwezo wake wa kuleta mabadiliko chanya.

'Israeli haitafanikiwa katika propaganda yake ya giza'

Amesema, mapambano makubwa ya kibinadamu dhidi ya mauaji ya Israeli yameonyeshwa na waandishi wa habari wanaofanya kazi katika eneo hilo, Altun amesema kwamba waandishi wa habari "sio tu wametoa taarifa lakini pia wamepigana katika mapambano matakatifu ya kuonyesha ukweli, na waandishi 119 wa Palestina wamekufa mashahidi katika jitihada hizo."

Juhudu zisizokuwa za kawaida za waandishi waliopo Gaza zimepelekea kuwepo kwa wimbi chanya la mabadiliko duniani kote, amesema.

"Sababu kwa nini Israeli imekuwa ikilenga kwa makusudi waandishi wa habari ni kwa sababu ya ukweli na msimamo wa haki wa waandishi ...Dunia nzima inajua kwamba Israeli kwa makusudi imelenga waandishi wa habari kama vile Wael al Dahdouh anaetafuta ukweli, kwa makusudi imeua familia yake." Ameongeza kwamba, Israeli inajaribu kuuwa ukweli na kuuziba pumzi."

"Haki pekee yake haitoshi, ni lazima kuwa bora zaidi. Tutapambana katika siasa, diplomasia, msaada wa kibinadamu, mawasiliano, na vyombo vya habari, kumaliza janga hili," ameongeza.

TRT World