Chama cha upinzani cha EFF cha Afrika Kusini kikiongozwa na Julius Malema kimefanya maandamano / Picha: EFF (X)

Chama cha upinzani cha Afrika Kusini Economic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema kilifanya maandamano katika Ubalozi wa Israel kwa mshikamano na watu wa Palestina siku ya jumatatu.

Malema amesema kuwa wamefanya maandamano kama mshikamano na Wapalestina kwani ulimwengu pia ulisimama na Afrika Kusini kukabiliana na ukoloni na ubaguzi.

"Tuko hapa Pretoria kitovu cha kupinga ubaguzi wa rangi ili kuandamana kwa sababu watu wa ulimwengu walisimama kwa mshikamano nasi Afrika Kusini wakati wa nyakati zetu ngumu. Hatuko huru mpaka Palestina iwe huru, Malema alisema.

Tumejumuika hapa nje ya Ubalozi wa Israel kwa sababu moja, kuwaambia Israeli Na ulimwengu kujua kwamba tunasimama na Palestina

Julius Malema. Picha: Reuters

Aidha, Malema ameishutumu vikali Israel kwa mauaji ya watu wa Palestina wasiokuwa na hatia na kupelekea uharibifu mkubwa.

"Tuna serikali ya aina gani katika Israeli ambayo hurusha mabomu hospitalini ambapo watu wametafuta kimbilio, ambapo watu kuna wagonjwa, na watoto na wanawake wajawazito," Malema alihoji.

"Ukiangalia nchi ya Palestina hakuna kitu kilichobaki cha ardhi ya Palestina."

Mzozo wa Gaza, ambao umekuwa chini ya mabomu ya Israeli na kuzingirwa kabisa tangu Oktoba 7, ulianza wakati kundi la Palestina la Hamas lilipoanzisha 'Operesheni ya Mafuriko ya Al Aqsa,' shambulio la mshangao lenye pande nyingi ambalo lilijumuisha mlipuko wa uzinduzi wa roketi na uingiliaji ndani ya Israeli kupitia ardhini, baharini na kwa njia ya anga.

TRT Afrika na mashirika ya habari