Mashirika ya Umoja wa mataifa yanaonya kuwa hali itazidi kuwa tete nchini Sudan Kusini bila hatua za haraka na uwekezaji katika kuisaidia nchi hiyo.
Viongozi wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) walitembelea Sudan kwa siku tatu.
Walitembelea jumuiya ambazo zinakabiliana na athari za matukio mabaya ya mabadiliko ya tabianchi pamoja na ukosefu wa miundombinu.
Maswala haya yanazidisha changamoto za kibinadamu nchini, kutishia mashamba na maisha ya wafugaji wa kilimo, na kuzilazimisha jamii za watu kuhama.
"Sudan Kusini ina uwezo wa kuzalisha chakula kingi zaidi katika Afrika Mashariki, changamoto ya mabadiliko ya tabianchi, miundombinu duni ya kilimo, kukosekana kwa utulivu, na misukosuko ya kiuchumi inaendelea kutatiza uzalishaji wa kilimo na mifugo na upatikanaji wa chakula,” Mkurugenzi Mkuu wa FAO Qu Dongyu alisema.
“Huku ikiwa ni asilimia nne tu ya mashamba yanayolimwa, na asilimia 80 ya vijana wake wanaoishi vijijini, kuna fursa kubwa ya kukuza na kuendeleza kilimo na sekta ya chakula kwa ujumla zaidi," rais wa IFAD, Alvaro Lario alisema.
"Ili kufanya hivyo tunahitaji kuhamasisha uwekezaji mkubwa na kutekeleza mbinu bora za kukabiliana na uhaba wa chakula na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Hii pia itaboresha sana ajira vijijini. Lakini tunahitaji kuchukua hatua sasa,” Lario aliongezea.
Hali ya kibinadamu kuzorota nchini Sudan Kusini inasababishwa na mchanganyiko wa migogoro, hali ya hewa, na kupanda kwa bei ya vyakula na mafuta.