Na Ibrahim Alegoz
Hivi karibuni, waziri wa Ulinzi wa Uturuki Yasar Guler na mwenzake kutoka Somalia, walikutana Ankara na kutia saini makubaliano ya kiulinzi na ushirikiano wa kiuchumi.
Mnamo Februari 21, Baraza la Mawaziri la Somalia liliidhinisha makubaliono hayo, yenye kuwezesha kuanzishwa kwa jeshi la pamoja la majini, huku Uturuki ikiwa tayari kutoa ulinzi kwenye bahari ya Somalia kwa muongo mmoja na kusaidia katika maendeleo ya rasilimali za baharini katika taifa hilo la Afrika.
Makubaliano hayo, sio tu kwamba yanalenga kuboresha mbinu za kiuchumi na usalama, lakini pia yana athari chanya kwenye ukanda huo, iwapo yataungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.
Ingawa, mititiriko ya rasimali haina mwisho na haina uendelevu, ni kipi kinapaswa kufanyika kuchangia usalama wa kikanda na pia kwa ustawi wa watu mara tu utakapotekelezwa?
Kwa muda mrefu sasa, pembe ya Afrika inatajwa kama eneo lenye umuhimu mkubwa katika siasa za nchi kubwa duniani, hasa wakati wa vita baridi, kutokana na kuwa eneo la kimkakati kwa nchi kubwa duniani.
Ingawa umuhimu wake wa kimkakati ulipungua kufuatia kumalizika kwa vita baridi, bado ulipata msukumo mpya kupitia vita vya kimataifa dhidi ya ugaidi.
Ukanda huo ni sehemu ya Bahari Nyekundu and Ghuba ya Aden katika mwambao wake, jirani na Saudi Arabia na Yemen ng'ambo ya mkondo, ambayo ni jia ya kuelekea Bahari ya Hindi na Bahari Nyekundu.
Pembe ya Afrika ilishuhudia baadhi ya vita vikali zaidi katika karne ya 20, kama vile vita vya Ethiopia-Somali vya 1977-78 na vita vya 1999-2000 vya mpaka wa Ethiopia-Eritrea mwanzoni mwa milenia.
Pengine hakuna tukio lolote la kisiasa katika eneo hilo lenye matokeo ya mageuzi kama kusambaratika kwa jimbo la Somalia mwaka 1991 kulivyoonyeshwa.
Kilichofuatia, kimetoa changamoto mbili ambazo ni usalama wa kimataifa: kuibuka kwa ugaidi kufuatia uingiliaji wa kijeshi wa Ethiopia nchini Somalia mwishoni mwa 2006 na tishio la uharamia katika pwani ya Somalia na Ghuba ya Aden.
Matukio haya mawili yanamaanisha kwamba, kwa njia moja au nyingine, ghasia zisizodhibitiwa hapo awali zinahusishwa na namna nguvu ilivyotumika kuleta utulivu.
Jumuiya ya Kimataifa imewekeza mabilioni ya fedha katika kuijenga upya Somalia toka mwaka 1991, na kutumia fedha nyingi katika kupambana na ugaidi na uharamia katika Ghuba ya Aden.
Bila shaka, ni mradi wenye changamoto za kutosha. Mara nyingi, jitihada zinazomilikiwa na ndani zinaendana na mbinu zinazoendeshwa na nje, na uwezekano wa mafanikio na kushindwa daima upo.
Licha ya changamoto zinazojitokeza, pengine ni wakati muafaka kuchunguza mbinu mbadala na kusonga mbele nchini Somalia.
Utafutwaji wa amani katika pembe ya Afrika
Mwaka 2011, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliutembelea mji mkuu wa Somalia, Mogadishu baada ya kukaribishwa na Rais wa wakati huo Sheikh Sharif, wakati nchi hiyo inakumbana na ukame na majanga ya kibinadamu yalioathiri mamilioni ya wa Wasomali.
Ziara hiyo inachukuliwa kuwa hatua ya mabadiliko machoni pa Wasomali, kwani ilikuwa ya kwanza kufanywa na kiongozi wa nchi isiyo ya Kiafrika tangu 1991.
Mnamo Februari 21, 2024, Rais wa Somalia Mahmoud alitoa taarifa baada ya mkutano wa baraza la mawaziri, “Somalia ina washirika na marafiki wengi ambao waliunga mkono juhudi zake za kurejesha uhai. Walakini, mmoja wa marafiki hao ambao wanastahili kutambuliwa maalum ni Uturuki, Uturuki imeiunga mkono Somalia na kuiepusha na baa la njaa ya mwaka 2011 na ziara ya Waziri Mkuu Erdogan ilikuwa muhimu.
Ziara hiyo ilifungua ukurasa mpya wa mahusiano baina ya nchi hizo mbili kuanzia karne ya 16. Tangu 2011, Uturuki imehamasisha mipango ya diplomasia ya kibinadamu hasa katika kukabiliana na mahitaji ya dharura ya kibinadamu ya watu wa Somalia, kama vile chakula, afya, na makazi.
Msaada wa kibinadamu ulifuatiwa na ule wa kiufundi na shughuli za kujenga uwezo ili kuinua mifumo ya serikali ya Somalia katika sekta mbalimbali.
Kwa mfano, mnamo Septemba 2017, kituo cha Mafunzo ya Kijeshi cha TURKSOM kilizinduliwa nchini Somalia kama sehemu ya mipango ya usalama, ambayo ni kipengele muhimu katika ujenzi wa serikali.
TURKSOM ilitoa mafunzo kwa jeshi la Somalia, lenye nia ya kurithi jukumu la kuimarisha ulinzi kutoka kwa majeshi ya Umoja wa Afrika.
Balozi wa Uturuki nchini Somalia, Mehmet Yilmaz –aliyehudumu kati ya 2018 na 2022 –na kuweka wazi kuwa Uturuki ilifikia hatua nzuri katika kutoa mafunzo kwa theluthi ya majeshi ya Somalia, yanayokadiriwa kuwa na askari kati ya 15,000 hadi 16,000.
Kabla ya hapo, Ubalozo mkubwa wa Uturuki ulifunguliwa Mogadishu, wakati wa utawala wa Rais wa sasa wa Somalia Mahmoud.
Mambo matatu makuu yanajitokeza katika mipango ya Uturuki katika ukanda wa Pembe ya Afrika. Taasisi za serikali na zisizo za kiserikali za Uturuki zinaunganisha misaada yao ya kibinadamu na kujenga uwezo, kuchangia usalama wa pwani ya Somalia kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama mwanachama mashuhuri wa NATO, ina jukumu muhimu katika mageuzi ya sekta ya usalama ya Somalia, na kudumisha ulinganifu na mkakati wa pande mbili.
Makubaliano ya hivi karibuni kati ya mataifa hayo mawili yanatoa picha nzuri ya historia ya miaka 13 ya uhusiano wa nchi hizo mbili.
Manufaa ya Somalia na kanda nzima
Makubaliano kati ya Uturuki na Somalia yana manufaa ya moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja kwa ajili ya uchumi wa Somalia, usalama wa pwani na kanda nzima kwa ujumla.
Ina uwezo wa kufungua mlango kwa mchakato mpana, ikiwa ni pamoja na usalama wa pwani, sekta ya rasilimali za maji na uvuvi, uboreshaji wa kisasa na maendeleo ya bandari, usafirishaji, usafirishaji, na sekta ya utalii, haswa suala la uharamia katika pwani ya Somalia.
Somalia ina pwani ndefu kabisa barani Afrika, ikiwa na urefu wa kilomita 3,898 kutoka Djibouti kwa upande wa Kaskazini na Kenya kwa upande wa kusini na ina utajiri wa ikolojia kwa upande wa magharibi wa Bahari ya Hindi.
Somalia pia ina eneo la kipekee la kiuchumi la takriban kilomita za mraba 1,000,000 lenye maili 200 za baharini nje ya nchi.
Hata hivyo, nchi hiyo bado haijavuna faida za utajiri wake wa rasilimali zake za baharini. Sababu kuu ni pamoja na uhaba wa miundombinu kwa ajili ya sekta ya uvuvi na huduma za vifaa na zaidi ya yote, masuala yanayohusiana na vipengele mbalimbali vya usanifu wa usalama.
Pamoja na kuwa na ukanda mrefu wa pwani na rasilimali kubwa ya bahari katika bara la Afrika, ukanda wa pwani wa Somalia bado unakabiliwa na uvuvi haramu na uhalifu.
Somalia inapoteza dola milioni 300 kwa mwaka kutokana na uvuvi haramu, wenye kutumia baruti na kuathiri maisha ya wavuvi wadogo.
Ingawa bado haijaendelezwa, sekta ya uvuvi ya kitaifa ni muhimu sana kwani inatoa chakula, riziki, mapato, na fursa za ajira kwa zaidi ya Wasomali 400,000 ambao wanajishughulisha moja kwa moja au kwa njia zisizo za moja kwa moja katika shughuli mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa uvuvi na huduma zinazohusiana.
Hata hivyo pamoja na hayo yote, kulingana na utafiti uliochapishwa na Taasisi ya Sera ya Urithi na Chuo Kikuu cha Mji wa Mogadishu, sekta ya uvuvi inazalisha dola milioni 135 kila mwaka, sawa na takriban asilimia mbili ya pato la taifa la Somalia.
Kwa hiyo, sekta ya uvuvi ina uwezo wa kuzalisha hadi dola milioni 500 kwa mwaka kwa thamani ya kuanzisha uchumi wa Somalia. Zaidi ya hayo, ikiwa itafikia uwezo wake endelevu, nchi inaweza kuvuna zaidi ya tani 200,000 za samaki kila mwaka.
Walakini, data ya serikali inaonyesha kuwa mnamo 2022, wavuvi wa eneo hilo walivua takribani tani 6,000 za samaki. Kwa upande mwingine, meli za kigeni za viwandani huvuna wastani wa tani 13,000 kila mwaka.
Kama sehemu ya ushirikiano wa Uturuki na Somalia, mapato yanayotokana na uwekezaji katika sekta ya jeshi la wanamaji na baharini yanapaswa kutoa mafunzo na vifaa kwa wavuvi wa Somalia, kuboresha miundombinu, na kuendeleza miradi mipya ya kulinda rasilimali za baharini.
Zaidi ya hayo, inaweza kukuza sekta ya uvuvi kwa kuvutia wawekezaji wa kigeni na kupata mapato endelevu ya mauzo ya nje.
Kwa muda mrefu sasa, uharamia umetishia kampuni za kimataifa za usafirishaji haswa zile zinazofanya kazi katika Ghuba ya Aden. Kulingana na kampuni ya uchakataji wa mafuta ya Vortexa, zaidi ya mapipa milioni 7.80 kwa siku ya shehena ya mafuta ghafi hupita katika mkondo huo katika miezi 11 ya kwanza ya 2023, kutoka mapipa 6.60 milioni kwa mwaka 2022.
Kulingana na shirika la takwimu la Statista, mashambulizi ya uharamia katika maji ya Somalia yalifikia kilele mwaka wa 2011, wakati matukio 160 yalirekodiwa, na kuongezeka hadi 358 katika kipindi cha miaka mitano kati ya 2010 na 2015. Idadi hii ilipungua hadi nane katika miaka saba kati ya 2016 na 2022. Ingawa takwimu zinaweza kuwa muhimu, wakati mwingine hazitoi taswira halisi.
Kulingana na ripoti ya 2010-2012 ya Bunge la Uingereza, "Operesheni za majini katika pwani ya Somalia zinagharimu karibu dola bilioni mbili kwa mwaka. Tatizo ni kwamba matumizi haya yanatibu tu ‘dalili za ugonjwa’ na hayafanyi chochote kushughulikia chanzo kikuu cha tatizo.” Gharama ya jumla ya uharamia, zaidi ya hayo, ilipanda hadi dola bilioni 7 mwaka 2011 pamoja na matumizi ya ziada.
Ni vyema kusisitiza kwamba dalili huwa zinajitokeza tena ikiwa sababu kuu hazijashughulikiwa vya kutosha. Makubaliano hayo yanapaswa kutarajiwa kuchangia pakubwa katika juhudi zinazoendelea za kimataifa kwa kuhakikisha usalama katika pwani ya Somalia na kufungua uwezo wa kiuchumi wa nchi za pwani.
Mwandishi wa maoni haya ana uhusiano na Chuo Kikuu cha Ibn Haldun, katika idara ya sayansi ya siasa na uhusiano wa kimataifa. Yeye ni mwandishi wa vitabu viwili : "Uingiliaji wa Kigeni na Uadilifu nchini Somalia: Jinsi na lini migogoro inabadilika kuwa vurugu" na "Sera ya Diplomasia ya Kibinadamu ya Türkiye nchini Somalia: Mbinu na Vyombo." Eneo lake la maslahi ni pamoja na ghasia za kisiasa, migogoro, uingiliaji kati wa kijeshi na Türkiye - Mahusiano ya Afrika kwa kuzingatia maalum Somalia.