Jeshi la Israeli siku ya Ijumaa limemshambulia mpiga picha wa Anadolu Alkharouf, ambae alikuwa katika majukumu yake katika eneo lililokaliwa la Jerusalem Mashariki. / Picha: AA  

Mkuu wa Jumuia ya Waandishi wa Habari wa Kimataifa (IFJ) amelaani vikali "kushambuliwa vibaya" kwa mpiga picha wa Anadolu Mustafa Alkharouf na vikosi vya Israeli.

"Ni jinamizi. Ni hali mbaya. Kwa hiyo, ni vigumu kusema mengi, zaidi ya kulaani," Anthony Bellanger ameiambia Anadolu Ijumaa.

"Nimeiangalia video na hasa Mustafa alikuwa akifanya kazi yake, na sio vyenginevyo, na nilipoangalia video, ilikuwa ni ya vurugu," Bellanger amesema.

Amesema kwamba, wakati akisubiri kupokea taarifa zaidi kuhusiana na hilo, IFJ inajaribu kumsaidia mpiga picha na kwamba atawapigia washiriki wake na waandishi wa Palestina Ramallah kumsaidia Alkharouf.

Kila siku, raia pamoja na waandishi wa habari, wamekuwa "wanalengwa na jeshi la Israeli," amesisitiza, na kuongeza kwamba angalau wapiga picha 64 na wafanyakazi wa vyombo vya habari wameuawa Gaza tangu Oktoba 7.

Amesema Jumuia hiyo inaweka taarifa ya matukio yote, ikiwemo uvamizi dhidi ya Alkharouf, kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

TRT World