Vikosi vya Israeli vimeshambulia waandishi wa habari wa TRT Arabi na waandishi wengine Jumapili mbele ya nyumba ya anaeshikiliwa Israa Al Jaabis huko Jerusalem.
Kufuatia shambulio hilo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Altun amesema, "Katika hali ya kutoheshimu sheria za kimataifa, Israeli, imeuwa waandishi wa habari hali inayogusa hisia za ulimwengu kwa kile kinachoendelea Gaza, na kuendelea kutumia mbinu ambazo hazikubaliki."
"Tunalaani serikali ya Israeli, ambayo sasa hivi imegeuza mashambulizi dhidi ya waandishi wanaotoa taarifa za kubadilishana kwa mateka katika eneo hilo na hata kuwashambulia kwa risasi za plastiki na kutumia vilipuzi vya kutoa machozi na mabomu ya machozi dhidi yao," aliandika katika ukurasa wa X Jumapili.
Israel sharti isitishe mashambulizi yake, hasa dhidi ya raia wa Palestina ambao hawana hatia, waandishi wa habari, wahudumu wa afya na wasaidizi wao, amesema, "Israeli sharti ifuate sheria za kimataifa." Amesema Kurugenzi ya Mawasiliano inafuatilia kwa karibu hali ya waandishi wa habari ambao wameshambuliwa na Israeli.