Umoja wa Mataifa unaonya kwamba vita nchini Sudan "vinahatarisha kusababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani huku raia wa nchi hiyo wakipambana waweze kuishi ndani ya mzozo huo.
Mamia ya wakulima wamehamishwa kutoka kwenye mashamba mazuri yenye rutuba, na hivyo kuongeza uwezekano wa ukame, Umoja wa Mataifa unasema katika ripoti yake.
Eddie Rowe, Mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani nchini Sudan, anasema kuwa nchi hiyo imebakiwa na pungufu ya asilimia 41 ya chakula tofuati na mwaka uliopita, wakati maeneo kama Darfur yakiripoti upungufu wa asilimia 78.
"Raia wa kawaida hana uwezo wa kujinunulia mahitaji muhimuThe average Sudanese does not have the purchasing power," Rowe told AFP, noting that 60 percent of the country was employed in the agricultural sector and that civil servants have not been receiving salaries.
"Watu takribani milioni tano hawana chakula," aliongeza.
Vita vya muda mrefu
Mapigano yalizuka mwaka jana kati ya jeshi la kawaida la Sudan, linaloongozwa na kiongozi mkuu wa nchi hiyo Abdel Fattah al-Burhan, na Vikosi vya Msaada wa Haraka vya kijeshi, vikiongozwa na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo.
Vita hivyo vimeua watu wengi na kuwafanya mamilioni wengine kuyakimbia makazi yao katika kile ambacho Umoja wa Mataifa imekiita "mgogoro mkubwa zaidi wa watu kuhama makwao duniani."
Halikadhalika imesababisha uhaba mkubwa wa chakula na mzozo mbaya wa kibinadamu ambao umewaacha watu wa nchi hiyo ya kaskazini mashariki mwa Afrika katika hatari ya njaa.
"Kuna jamii zilizo hatarini kila mahali ambazo zinahitaji usaidizi," alisema Rein Paulsen, mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo idara ya dharura.
'Kulala njaa'
Kulingana na utafiti wa kituo cha Fikra, ni asilimia 37 pekee ya ardhi ya kilimo ambayo bado inalimwa kote Sudan, kulingana na kituo cha utafiti cha Fikra.
Katika eneo lililokuwa na rutuba la Al-Jazira pekee, mapigano tayari yameacha kutumia hekta 250,000 za ardhi, na kufyeka takriban asilimia 70 ya uzalishaji wa kila mwaka wa ngano nchini humo wa tani 800,000.
"Msimu mkuu wa upanzi huanza katika wiki chache tu. Mwezi wa Juni ni mwezi muhimu kwa wakulima kupanda mazao muhimu kwa mwaka," alisema Paulsen.
Vifaa ya haraka
Uzalishaji wa chakula umesimama kwani barabara zote zinazoelekea Bandari ya Sudan, kituo kikuu pekee cha kuingilia zimekatika.
"Makampuni mengi yanayosambaza mbolea na viuatilifu yamefungwa," alisema Mohamed Suleiman, mkulima wa mahindi kutoka jimbo la mashariki la Gedaref.
Vita hivyo, ambavyo wataalam wameonya kuwa vinaweza kudumu kwa miaka -- vimewahamisha Wasudan milioni 18 katika uhaba mkubwa wa chakula, milioni tano kati yao wako katika hatari ya njaa.
Jumuiya ya kimataifa mapema mwezi huu iliahidi msaada wa zaidi ya euro bilioni mbili kwa Sudan, nusu tu ya kile ambacho Umoja wa Mataifa ulidai, wakati wa mkutano mjini Paris.