Umoja wa Afrika na mapinduzi ya serikali barani Afrika

Umoja wa Afrika na mapinduzi ya serikali barani Afrika

Kulikuwa na tukio la mapinduzi ya serikali nchini Niger Jumatano tarehe 28 Julai
Umoja wa Afrika unapinga mapinduzi ya serikali kwa njia ambayo si ya uchaguzi / Photo: Reuters

Nchini Niger, Magharibi mwa Afrika hali ni ya sintofahamu huku rais akiendelea kushikiliwa na wanajeshi ambao wanadai wamemuondoa madarakani .

Mapinduzi ya serikali hufanyika wakati kikundi au watu wanaamua kumuondoa kiongozi wa serikali kwa madarakani.

Barani Afrika kumekuwa na mapinduzi 16 ambayo yamefaulu na mengine yalizimwa kabla ya marais kuondolewa katika kiti chao .

Chad, Mali, Sudan, Burkina Faso na Guinea na sasa Niger iko chini ya utawala wa kijeshi. Mahamat Deby afisa wa kijeshi alichukua uongozi nchini Chad Aprili 2021 mara tu baada ya kifo cha baba yake rais wa wakati huo Idris Deby.

Mnamo Agosti 2020 na Mei 2021 Mali ilipitia mapinduzi. Ilifuatiwa na Guinea mnamo Septemba 2021 na Burkina Faso Januari 2022.

kikundii cha wanajeshi nchini Niger walitangaza kumuondoa rais 26 Julai 2023 

Tangu Januari 2021 wakati jeshi lilipompindua rais wa wakati huo wa Sudan Omar El Bashir, nchi hiyo haijarejea katika utawala wa kiraia.

Nchini Niger kundi la wanajeshi walidai kuwa ndio rais wa nchi hiyo na wamekuwa wakimshikilia yeye na familia yake tangu tarehe 26 Julai 2023.

Umoja wa Afrika umezisimamisha Mali, Sudan, Burkina Faso na Guinea kutoka kwa shughuli zozote za Umoja wa Afrika hadi zitakaporejea katika utawala wa kiraia kupitia uchaguzi.

Vyanzo vya mapinduzi ya serikali

Kudorora kwa mchakato wa demokrasia barani humo, viongozi kutoheshimu matakwa yao ya kikatiba, kushindwa kwa baadhi ya watu kuheshimu matokeo ya uchaguzi kumetajwa kuwa baadhi ya vichochezi vya mapinduzi.

AU inasema kuna "ongezeko la idadi ya Nchi Wanachama ambazo zinaendesha michakato ya kidemokrasia kurekebisha na kuondoa ukomo wa mihula ya kikatiba, wakati zingine zinapinga juhudi za kuweka ukomo wa muda katika Katiba zao"

Umoja wa Afrika Umeonya "umeonya wale wanaofadhili mapinduzi, wapiganaji wa kigeni na mamluki katika nchi wanachama wake kwamba vitendo vyao vichafu havitavumiliwa".

Aidha tamaa ya wanajeshi kuonja uongozi pia umepeleka mapinduzi kutendeka.

Mahamat Deby afisa wa kijeshi alichukua uongozi nchini Chad Aprili 2021 baad aya kifo cha babake aliyekuwa rais wa nchi hiyo /Picha Getty 

Umoja wa Afrika unasema mabadiliko ya serikali kinyume na katiba, kwa hali yoyote ile, hayafai kuhalalishwa.

Viongozi wa Afrika katika mkutano wao wa Aprili 2022 kuhuku mapinguzi ya serikali walionya "wale wanaofadhili mapinduzi, wapiganaji wa kigeni na mamluki katika Nchi Wanachama kwamba vitendo vyao vichafu havitavumiliwa."

Lakini mwaka moja baadaye Umoja wa Afrika umepatwa na changamoto mpya, mageuzi ya serikali nchini Niger .

TRT Afrika