UN Yasema kuwa  wanawake huficha unyanyasaji wa kijinsia ili kuepuka unyanyapaa./ Picha : AA

Pande zinazohusika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan tangu Aprili 2023 zimeshutumiwa kutumia unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji kama silaha ya vita.

Mona Rishmawi, mjumbe wa jopo huru ya Umoja wa kimataifa juu ya Ukweli na haki kuhusu Sudan, alitoa maoni yake kuhusu ripoti za unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake nchini Sudan wakati wa mahojiano na Anadolu.

Rishmawi alisema kutokana na mzozo huo, wanawake wengi wamekuwa wakimbizi na wanawake wengi pia wamelazimika kusafiri kwenda nchi nyingine peke yao kwa sababu waume zao waliuawa.

''Wanawake wa Sudan mara kwa mara wamefurushwa na kukabiliwa na hatari mbalimbali wakati wa safari zao,'' alisema.

"Kuna visa vingi vya watu kupotea. Wengi hawajui hatima ya wapendwa wao. Walihama mara nyingi ndani na nje," alisema.

Waathiriwa wanyanyapaliwa

Rishmawi aliongeza kuwa familia mara nyingi huwa na watoto wengi, na wanawake huachwa kuwatunza peke yao.

Rishmawi alisema ukiukwaji dhidi ya wanawake katika mzozo huo umeenea sana ambao unaripotiwa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa.

Alieleza kwa kina kuwa wanawake wanakabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia wakati wakikimbia makazi yao na wale wanaozuiliwa wakati wa uhamiaji pia wanakumbana na ukatili wa kijinsia.

Akisisitiza wanawake na wasichana wanalengwa na kuadhibiwa kutokana na majukumu yao katika jamii, alisema, "Wanawake wa Sudan ambao walijaribu kusaidia wengine wanaohitaji pia wamekabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia."

Rishmawi aliripoti kuwa wanawake huficha unyanyasaji wa kijinsia ili kuepuka unyanyapaa.

Vita vya Sudan vimeendelea kwa zaidi ya miezi kumi na tano sasa bila matumaini yakupatikana upatanishi au usitishaji vita.

Mazungumzo ya amani yanayofadhiliwa na Marekani na saudi Arabia yanafanyika mjini geneva yanayo hudhururiwa na wapiganaji wa jeshi la dharura RSF, japo upande wa jeshi la taifa umekataa kuhudhuria.

AA