Jacob Zuma ameonesha nia ya kugombea kupitia chama cha uMkhonto we Sizwe (MK), chama kipya nchini Afrika Kusini. / Picha: Getty 

Tume ya Uchaguzi ya Afrika Kusini imesema kuwa imekata rufaa katika mahakama hiyo ya juu ya nchi hiyo kujua iwapi Rais wa zamani Jacob Zuma atagombea tena kwenye uchaguzi wa mwezi Mei.

Siku ya Ijumaa, tume hiyo ilisema kuwa imepeleka rufaa ya dharura na ya moja kwa moja kwenye Mahakama ya Kikatiba ili kupata "ufafanuzi wa suala hilo."

Ni mabadiliko ya hivi punde katika mzozo wa kisheria kuhusu sifa ya Zuma mwenye miaka 81 kupitia chama kipya cha Umkhonto we Sizwe (MK).

Katika maamuzi ya kushangaza yaliyotolewa siku ya Ijumaa, mahakama hiyo ilisema kuwa Zuma ana sifa ya kugombea katika uchaguzi huo.

Sababu za kuondolewa

Chombo hicho kiliondoa jina la Zuma kwenye kinyang'anyiro hicho, kikisema katiba inazuia mtu yeyote aliyehukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi 12 jela.

Zuma alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela mnamo Juni 2021 baada ya kukataa kutoa ushahidi mbele ya jopo lililokuwa likichunguza tuhuma za ufisadi dhidi yake.

Mawakili wake walisisitiza kuwa hukumu hiyo haikumwondolea sifa kwani ilifuata kesi za madai badala ya jinai na ilifupishwa kwa kusamehewa.

Zuma aliachiwa huru kwa msamaha wa kimatibabu, miezi miwili tu baada ya kuingia kifungoni.

Ufafanuzi unahitajika

Tume ya uchaguzi ilisema Ijumaa kulikuwa na "maslahi makubwa ya umma katika kutoa uhakika juu ya tafsiri sahihi" ya kifungu cha katiba kinachohusiana na wagombea ambao wamepatikana na hatia.

"Ni muhimu kupata ufafanuzi huo kwa ajili ya uchaguzi ujao," iliongeza.

Uchaguzi mkuu wa Afŕika Kusini unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa zaidi tangu ujio wa demokrasia mwaka 1994, haswa kutokana na uwepo wa Zuma.

Kutokana na umaarufu wake, chama cha MK kinatarajiwa kupunguza uwiano wa kura wa chama tawala cha African National Congress (ANC), anapotokea Rais huyo wa zamani.

Hii inaweza kuharakisha ANC kupata mgao wake wa kura ukishuka chini ya asilimia 50 kwa mara ya kwanza tangu 1994.

Itawalazimu kuungana ili kubaki madarakani, ikitokea wakipata nafasi bungeni.

TRT Afrika