Tukio hilo lilitokea katika eneo la Kisiwapanza, Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba./Picha: TRT Afrika.

Idadi ya vifo vilivyotokana na kula nyama ya Kasa sasa imefikia 9 huku waliofikishwa hospitalini wakiwa bado hawajaruhusiwa.

Mmoja wa waandishi wa habari wa eneo hilo, ameiambia TRT Afrika kuwa mtu mmoja zaidi amefariki dunia wakati anapokea matibabu hospitalini, kufuatia tukio hilo lililotokea Machi 5, katika eneo la Kisiwapanza, Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba.

Kulingana na mwanahabari huyo, watu wengine 98, bado wanaendelea kupokea matibabu hospitalini kufuatia kula Kasa wanaodhaniwa kuwa na sumu.

Mmoja wa ndugu walioathirika na tukio hilo akiwa katika hali ya maombolezo./ Picha:TRT Afrika

Katika miaka ya hivi karibuni, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imepiga marufuku uvuvi wa samaki aina ya Kasa kwa kile kilichoelezwa kuwa viumbe hao kutokuwa salama kutokana na mabadiliko ya vyakula wanavyokula na kusababisha sumu ya mwili na kuhatarisha uhai kwa binadamu anayekula nyama husika.

Tafiti mbalimbali zimebaini kwamba kasa wamekuwa wakila chakula aina ya majani yenye mchanganyiko wa sumu ambayo binadamu akila nyama yake husababisha kifo.

TRT Afrika