Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa./Picha:Wengine

Kesi inayomkabili aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibrod Slaa imesogezwa mbele hadi Januari 17, 2025.

Dkt. Slaa anatuhumiwa kwa madai ya kusambaza taarifa za uongo katika mtandao wa X, zamani Twitter.

Mwanasiasa huyo ambaye pia amewahi kuhudumu kama Balozi wa Tanzania nchini Sweden na Denmark, Finlad na Norway, alifikishwa mahakamani hapo Januari 10, 2025 na kusomewa kesi ya jinai namba 993 ya mwaka 2025.

Dkt. Slaa anadaiwa kutenda kosa hilo chini ya kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao namba 14 ya mwaka 2015.

TRT Afrika