Khartoum wakati wa vita | Picha: AA

Sudan siku ya Jumatatu iliongeza muda wa kufungwa kwa anga ya nchi hiyo hadi Agosti 15 huku kukiwa na mapigano yanayoendelea kati ya jeshi na kundi la wanamgambo la Rapid Support Forces (RSF).

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ilisema anga ya Sudan itafungwa kwa safari zote za ndege hadi Agosti 15, Shirika rasmi la Habari la Sudan lilisema.

Ni misaada ya kibinadamu pekee na safari za ndege za uokoaji zitakazoruhusiwa kusafiri, iliongeza.

Sudan imeharibiwa na mapigano kati ya jeshi na RSF tangu Aprili, katika mzozo ambao uliua zaidi ya raia 3,000 na kujeruhi maelfu, kulingana na ripoti za matabibu za ndani.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) linakadiria kuwa karibu watu milioni tatu wamekimbia makazi yao kutokana na mzozo wa sasa nchini Sudan.

AA