Sudan imemrejesha nyumbani balozi wake nchini Kenya baada ya Kenya kuandaa mkutano wa wanajeshi wa RSF./Picha: AA

Nchi hiyo imemrudisha nyumbani balozi wake wa Kenya baada ya Kenya kuwa mwenyeji wa mkutano wa wanajeshi wa RSF.

Sudan imemrejesha nyumbani balozi wake nchini Kenya baada ya Kenya kuandaa mkutano wa wanajeshi wa RSF.

Wizara ya Mambo ya Nje imemwita balozi wake kwa ajili ya mazungumzo baada ya Kenya kuwa mwenyeji wa mkutano wa wanajeshi wa RSF," limesema Shirika la Habari la SUNA.

Katika mkutano uliofanyika jijini Nairobi mapema wiki hii, wanajeshi wa RSF walieleza nia yao ya kuanzisha serikali yao.

Katika taarifa yake ya awali, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ilimlaumu Rais William Ruto wa Kenya kwa hatua hiyo ya kudharau utawala wa Sudan.

Kulingana na chanzo kimoja cha RSF, mpango huo ambao ulikuwa uidhinishwe siku ya Jumanne, umesogezwa mbele mpaka mwishoni wa wiki hii.

Vita kati ya Jeshi la Sudan na RSF vilivyoanza Aprili 2023, vimegharimu maisha ya maelfu ya watu na kuwaacha zaidi ya milioni 12 bila makazi.

TRT Afrika