Filamu ya Black Panther: Wakanda Forever ilivuma sana na kupata umaarufu. Picha: Marvel Studios

Muigizaji wa filamu maarufu "Black Panther: Wakanda Forever" M’Baku, majina rasmi Winston Duke, aliyeigiza kama kiongozi wa kabila la Jabari katika filamu hiyo, ameidhinishwa rasmi kuwa raia wa Rwanda.

Winston Duke akila kiapo. Picha: RBA

Winston Duke alikula kiapo akiwa nchini Rwanda aliposhiriki makala ya 19 ya sherehe za kumpa jina sokwe maarufu KwitaIzina. Winston Duke na muigizaji mwenza, Danai Gurira, wa filamu maarufu ya Black Panther, waliwapa sokwe majina ya Aguka T’Challa na Intarumikwa yaani jitu mstahimilivu.

Rais Paul Kagame akiwa na wageni wake, Ikulu ya Rwanda. Picha: Ikulu ya Rwanda

Winston Duke, aliyezaliwa kwenye kisiwa cha Trinidad na Tobago, kilichoko kaskazini-mashariki mwa Amerika Kusini, alisoma katika Shule ya Kuigiza ya Yale, ambapo alikutana kwa mara ya kwanza na muigizaji wa Kenya, Lupita Nyong’o wakati Duke alipokuwa mwanafunzi mpya naye Nyong’o akiwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza aliyepewa kazi ya kumsaidia Duke.

Muigizaji wa filamu maarufu "Black Panther: Wakanda Forever" M’Baku, majina rasmi Winston Duke. Picha: Marvel Studios

Aliigiza kama nyota wa soka ambaye anafanya uhalifu wa chuki katika filamu; Law & Order: SVU, kiongozi wa genge ndani ya filamu Person of Interest, mchezaji wa soka katika tamthilia za Modern Family, Avengers: Endgame, Avengers: Infinity War,' na filamu mbalimbali.

Duke alichagua kumpa mtoto wake sokwe jina "Intarumikwa", ambalo tafsiri yake ni "Resilient Giant" (jitu linalostahimili) kwa heshima ya marehemu mama yake ambaye alikuza maadili ya uhifadhi ndani yake.

TRT Afrika