Somalia yapiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki

Somalia yapiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki

Serikali imewataka wajasiriamali kutafuta njia mbadala na rafiki kwa mazingira.
Somalia imepiga marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia angaza kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia mwisho wa Juni/ picha : Wengine 

Somalia imetangaza kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia mwisho wa Juni, 2024.

Wizara ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabia nchi ilisema kuwa Somalia imepiga marufuku uingizwaji, usafirishaji, biashara, na matumizi ya mifuko ya aina hiyo, ifikapo mwisho wa mwezi wa sita.

Kwa namna ya pekee, wizara pia imewataka wajasiriamali na makampuni nchini Somalia kubuni njia mbadala za mifuko ya plastiki ambayo hazina madhara kwa mazingira.

Wataalam wanasema mifuko ya plastiki imekuwa chanzo kikuu cha uchafuzi wa mazingira na kwa kiasi kikubwa imechangia kuua wanyama wa nchi kavu na wale waishio baharini. Picha: Getty 

Watetezi wa kupinga mabadiliko ta tabia nchi na wanaharakati wa mazingira wamekaribisha uamuzi huo.

Maisha ya ardhini na baharini

Mwakilishi mkazi wa taasisi ya Nordic Support, Kassim Gabowduale amesema kwa kiasi kikubwa, mifuko ya plastiki iliyotumika, imechangia uharibifu wa mazingira na kusababisha kukatisha uhai wa viumbe vya nchi kavu na baharini.

Kulingana na Gabowduale, katazo hilo litapunguza uchafuzi wa mazingira nchini Somalia.

"Hii ni hatua ya wakati muafaka kwani itaokoa maisha katika nchi kavu na mazingira ya baharini," alisema.

Hata hivyo, Abdullahi Hassan ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Action for Climate Change (CACC), amesema, katazo hilo limechelewa, hasa kutokana na athari za mifuko ya plastiki kwenye mazingira.

Hassan alisema ukosefu wa uelewa na ufahamu wa madhara ya uchafuzi unaotokana na mifuko ya plastiki unaweza kuchelewesha hatua hizo.

Ahadi ya dola milioni 10

Mifuko hii huenea kwa kasi kwa njia ya upepo na maji, hasa katika makazi ya watu, mashambani na katika vyanzo vya maji.

“Taka hizi zinachafua mazingira, zikiwemo fukwe, mito na maeneo ya kilimo. Plastiki hizo zimekuwa na athari mbaya kwa mazingira nchini,” aliongeza Hassan.

Somalia imekuwa ikifanya kazi katika kujenga hatua za kulinda baionwai zake.

Mwaka 2023, Rais Hassan Sheikh Mahamud alitoa dola milioni 10 katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kulinda baionwai za nchi hiyo.

Afrika inazidi kukabiliwa na majanga ya hali ya hewa, ingawa inachangia asilimia 4 tu ya gesi chafu zote zinazozalishwa duniani.

TRT Afrika