Siku ya Wazazi Duniani ni tarehe 1 juni | Picha: TRT Afrika

Nchi 36 zilizofanyiwa utafiti na shirika la utafiti la Afrobarometer mwaka 2021/2022, sita kati ya watu wazima 10 (61%) wanasema wazazi "wakati mwingine" au "daima" wana haki ya kutumia nguvu za kimwili kuwatia nidhamu watoto wao.

Ni 38% tu ya waliohojiya wanasema adhabu ya viboko "haifai kamwe".

Wengi wanasema kumpiga mtoto ni muhimu na kukubalika katika baadhi ya nchi nchi - 28 kati ya 36. Karibu tisa kati ya 10 nchini Benin (88%), Cameroon (87%), Burkina Faso (86%), na Niger (85%). Miongoni mwa waliohojiwa wenye umri wa miaka 18-25, 60% wanakubaliana na tendo la kumpiga mtoto.

Malawi, Lesotho, na Tanzania hawakubaliani na matumizi ya ubavu kuwaelekeza na kuwaadhibu watoto wao: 72% - 74% wanaona kuwa "haina haja".

Upinzani dhidi yake ni mkubwa miongoni mwa watu wazima walio na angalau elimu ya shule ya msingi (40% -41%) kuliko wale ambao hawana elimu rasmi (29%).

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema adhabu ya viboko kwa watoto haina "matokeo chanya," inadhuru maendeleo ya watoto na inapaswa kusitishwa.

Siku ya Wazazi Duniani ni leo tarehe 1 Juni, kila la kheri.

TRT Afrika