Mnamo Aprili, mapigano yaliyozuka katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum yalisambaratisha kabisa mji huo, kusababisha vifo vya maelfu ya watu huku mamilioni wengine wakiachwa bila makao.
Vita hivi ni kati ya jeshi la taifa na wapiganaji wa kikosi cha Masaada wa Haraka, RSF, juu ya uongozi wa nchi.
Haya ndio matukio kama yalivyojiri
Aprili 15 - Baada ya wiki kadhaa za mvutano kuhusu mpango wa kukabidhi madaraka kwa raia, mapigano makali yalizuka katika mji mkuu Khartoum na miji mingine ya karibu.
Aprili 16 - Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP linatangaza kusitisha kwa muda shughuli zake nchini Sudan, baada ya wafanyakazi wake kuuawa
Aprili 22 – Balozi za kigeni zawahamisha wafanyakazi wao na raia wa kigeni nchini Sudan.
Mei 20 - Makubaliano ya siku 7 ya kusitisha mapigano kufuatia upatanishi wa Saudi Arabia na Marekani mjini Jeddah. Mazungumzo yalivunjika mwezi Juni.
Mei 29 – Idadi ya wakimbizi na walioachwa bila makao yafikia Milioni 1.4. Idadi hiyo iliongezeka hadi Milioni 3.5 (UNHCR)
Juni 19 – Jamii ya kimataifa yaahidi msaada wa $1.5 Bilioni kusaidia Sudan na majirani zake katika kikao cha Geneva, ikiwa ni nusu ya fedha zinazohitajika kukabili janga la kibinadamu.
Julai 10 – IGAD imependekeza kupelekwa kikosi cha kuweka amani Sudan. Sudan ilikataa pendekezo hilo mara moja.
Julai 13 – Misri ilianzisha upatanishi mpya kati ya pande zinazo zozana Sudan katika kikao mjini Cairo wa viongozi wa nchi jirani wa Sudan.