Shambulio la Israel lililoua familia ya mwandishi wa Aljazeera ni la 'kutisha'

Shambulio la Israel lililoua familia ya mwandishi wa Aljazeera ni la 'kutisha'

Shambulio jengine la kutisha kwa uhuru wa habari linaonyesha vitimbi vinavyoendelea vya Israel.
Altun ametaka kusitishwa kwa mapigano mara moja na majadiliano ya kubadilishana kwa wafungwa, akitilia msisitizo wa kuruhusiwa kwa msaada wa kimataifa wa kibinadamu kuingia Gaza. Picha/AA

Uturuki imelaani shambulio la Israel dhidi ya waandishi wa Palestine Gaza and familia zao kufuatia mauaji ya familia ya mwandishi wa Al Jazeera.

"Tumeshangazwa na tukio jengine dhidi ya waandishi, ambapo nyumba ya mwandishi wa Al Jazeera, Wael A l Dahdouh imeshambuliwa na Israel." Mkurungezi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun amesema katika mtandao wa kijamii wa X siku ya Jumatano.

Altun alitoa rambirambi zake na kuonyesha masikitiko yake kwa Al Dahdouh.

Ameongeza, "Inatuwia vigumu kuamini kwamba hili lilikuwa shambulio la bahati mbaya, huku Israel ikijaribu kuficha ukweli kuonekana Gaza. Mashambulio haya ni njama za kigaidi za kuwanyamazisha waandishi."

Mashambulizi yasiochagua

Wakiendelea na njama za unyanyasaji na vitisho kwa raia, baadhi ya maafisa wa Israel wanathubutu kuikosoa Uturuki kuhusu msimamo wake juu ya Gaza, kwa mujibu wa Altun ambae pia alisema "Hatutahubiriwa na mtu yeyote kuhusu ugaidi ni nini. Tumekuwa tukipambana na makundi ya kigaidi kama PKK na Daesh kwa muda mrefu. Hakuna kinachokubalika kimataifa kwa kushambulia raia."

Altun pia amesisitiza kuwa, dunia nzima imeona sio tu shambulio la Oktoba 7 dhidi ya miji ya Israel lakini pia mashambulizi ya Israel dhidi ya raia wa Gaza ambayo yamesababisha vifo vya watu 6,000 mpaka sasa. Kuwazingira mamilioni ya wananchi bila kuwepo kwa misaada ya kibinadamu katika hali ya kikatili na kudhalilisha.

TRT Afrika