Maandamano hayo yalikuwa ni ishara ya kuunga mkono jeshi la DRC ambalo linapambana kurejesha mji wa Goma ambao kwa sasa umetwaliwa na kikundi cha waasi cha M23./Picha: @newvisionwire

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini DRC imesikitishwa na kitendo cha waandamanaji kuvamia na kuharibu balozi mbalimbali jijini Kinshasa.

Katika taarifa yake iliyotolewa siku ya Jumanne Januari 28, 2025 saa chache baada ya kutokea kwa uharibifu huo, serikali ya nchi hiyo imeeleza kusikitishwa na vitendo hivyo, huku ikiahidi kuwa jitihada za lazima zitafanyika kuwalinda maofisa wa ubalozi wa nchi mbalimbali ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na mali zao.

Kulingana na Wizara hiyo, ulinzi umeimarishwa katika balozi kadhaa kufuatia uvamizi na uharibifu wa ofisi za Ubalozi wa Kenya, Uganda, Rwanda, Marekani, Ufaransa, Ubelgiji pamoja na ofisi ya Umoja wa Mataifa.

Januari 28, picha mbalimbali ziliwaonesha mamia ya waandamanaji, wakivamia na kufanya uharibifu kwenye balozi hizo jijini Kinshasa.

Maandamano hayo yalikuwa ni ishara ya kuunga mkono jeshi la DRC ambalo linapambana kurejesha mji wa Goma ambao kwa sasa umetwaliwa na kikundi cha waasi cha M23.

TRT Afrika